UFARANSA-FILLON-SIASA

Kamati ya chama cha Republican yamuunga mkono François Fillon

Rais wa Baraza la Seneti Gerard Larcher akiwa pia Mwenyekiti wa Kamati ya Kisiasa ya chama cha Republican, Machi 6.
Rais wa Baraza la Seneti Gerard Larcher akiwa pia Mwenyekiti wa Kamati ya Kisiasa ya chama cha Republican, Machi 6. GABRIEL BOUYS / AFP

Kamati ya kisiasa ya chama cha Republican imekutana Jumatatu wiki hii, kuamua hatima ya mgombea wa chama hicho François Fillon. Kwa kauli moja, Kamati hiyo imeamua kumuunga mkono François Fillon.

Matangazo ya kibiashara

Awali kura za maoni zilionyesha, kuwa asilimia 70 ya wapigaji kura, wanataka atoke katika mashindano hayo.

"Kamati ya kisiasa ya chama cha Republican, baada ya kutathimini hali inayojiri wakati huu kuhusu mgombea wa chama hiki, imemuunga mkono kwa kauli moja François Fillon, " Gérard Larcher, Mwenyekiti wa taasi hiyo ameviambia vyombo vya habari, baada ya mkutano Kamati ya kisiasa ya chama cha Republican.

Uamuzi huo unakuja siku moja baada ya François Fillon kukutana na wafuasi wake katika eneo la Trocadero katika mji wa Paris. Mkutano huo wa hadhara ulifanyika katika jaribio la mwisho, kuonesha kuwa uchunguzi kuhusu uhalifu, anaomkabili, hautomzuwia kushinda katika uchaguzi wa rais.

François Fillon alifanya mkutano wake huo siku ya Jumapili. Ili aweze kukabiliana na shinikizo ya viongozi wa kambi yake ambao wanataka kumshinikiza ajiuzulu katika kinyang'anyiro hicho, alihitaji kupata angalau watu 50.000 katika mkutano huo wa hadhara uliofanyika katika eneo la Place du Trocadero.