Canard Enchaîné: François Fillon alisahau kutangaza mkopo wa euro 50,000

François Fillon (kushoto) karibu na Marc Ladreit de Lacharrière (kulia), akimkopa EUR 50 000 mwaka 2013 (picha ya zamani).
François Fillon (kushoto) karibu na Marc Ladreit de Lacharrière (kulia), akimkopa EUR 50 000 mwaka 2013 (picha ya zamani). FRANCK FIFE / AFP

Kwa mujibu wa gazeti la kila wiki la Canard Enchaîné, François Fillon alipokea mwaka 2013 kutoka kwa mfanyabiashara Marc Ladreit de Lacharrière mkopo wa Euro 50 000, bila riba na haukutangazwa kwenye Mamlaka ya nchi (HATVP).

Matangazo ya kibiashara

Bw Ladreit de Lacharrière amethibitisha kuwa alitoa mkopo huo bila riba, na kuongeza kuwa alilipwa. "Kusahau" kutangaza mkopo huu "kunaweza kumueweka hatarini mgombea urais," gazeti hili la kila wiki limeongeza. Kwa mujibu wa Kanuni ya Kodi, mkopo wowote ule ulio juu ya Euro 760 unapaswa kutangazwa na yule mkopaji.

Katika toleo lake Jumatano wiki hii, Canard Enchaîné imeaonyesha kwamba majaji wanaohusika na uchunguzi unaomlenga François Fillon wanashughulikia suala la mkopo ambao haukutangazwa wa Euro 50,000 ulitolewa mwaka 2013 kwa mgombea wa mrengo wa kulia. Mkopo ambao ulitolewa na rafiki yake Marc Ladreit de Lacharrière , mmiliki wa gazeti la Deux Mondes.

Kwa mujibu wa gazeti la kila wiki, François Fillon hajatangaza mkopo bila riba au tarehe ya mwisho ya kulipa mkopo huo alipotangaza mali zake, tangazo ambalo aliliwasilisha kwenye Mamlaka ya nchi (HATVP).

Wakili wake, Antonin Levy, amethibitisha kwenye runinga ya BFM kuwepo kwa mkopo huo ambao "alisahau" kutangaza. "Alisahau alipotangaza mali zake," Antonin Levy amesema.

"Huu ni mkopo ambao ulilipwa. Hakuna hoja," amesema, akiongeza kuwa François Fillon aliwahi kuelezea mkopo huo " kwa wachunguzi.

Mfanyabiashara Marc Ladreit de Lacharrière amethibitisha upande wake kua alitoa mkopo huo, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wakili wake, Emmanuel Brochier, ambaye aliliambia shirika la habari la AFP. "Deni hili limekuwepo na lilipwa. Hakuna shida yoyote, "amesema mwanasheria wa Mkurugenzi Mkuu wa Fimalac, aliye karibu na mgombea wa mrengo wa kulia katika uchaguzi wa urais. Mwanasheria huyo hakutaja sababu na tarehe ya mkopo, ambao ulianza mwaka 2013, kwa mujibu wa gazeti la kila wiki la Canard Enchaîné.