KOREA KUSINI-SIASA-UCHUMI

Korea Kusini: Park Geun-hye aondoka Ikulu

Park Geun-hye, muda mfupi kabla ya kuwasili kwake katika makazi yake binafsi, Machi 12, 2017.
Park Geun-hye, muda mfupi kabla ya kuwasili kwake katika makazi yake binafsi, Machi 12, 2017. Seo Myeong-gon/Yonhap via REUTERS

Nchini Korea ya Kusini, rais wa zamani Park Geun-hye hatimaye ameondoka ikulu, kuelekea nyumbani kwake siku mbili baada ya kutimuliwa madarakani.

Matangazo ya kibiashara

Park Geun-hye alikuwa amejificha ikulu kwa masaa arobaini na nane akikataa kuondoka wakati ampao angelikua aliondoka tangu Ijumaa Machi 10.

Wakati huo huo rais aliyetimuliwa madarakani, amjieleza hadharani kwa mara ya kwanza, hutuba ambayo ilijaa maneno ya dharau.

Mamia ya wafuasi wake, wakiwa na bendera mkononi, walisubiri gari nyeusi la kifahari lililokua likimsafirisha Park Geun-hye nyumbani kwake, katika eneo wanakoishi matajiri kusini mwa mji wa Seoul. Polisi elfu moja walitumwa kwa ajili ya tukio hilo. Akizungukwa na walinzi, huku akitabasamu,rais aliyetimuliwa mamlakani, aalisalimiana na wafuasi wake, ambao walikua wakisema "Futeni uamuzi wa kumng'atua madarakani! ".

Katika taarifa iliyosomwa na mmoja wa wasemaji wake, wake Park Geun-hye alitoa shukurani zake kwa wafuasi wake na kuomba radhi kwa kutofikia mwisho wa muhula wake. "Hata kama itachukua muda, nadhani ukweli utajulikana," Park Geun-hye ameongeza.

Kauli yenye utata

Park Geun-hye anaonekana kukataa kutambua uamuzi wa Mahakama ya Katiba wa kumtimua madarakani. Kauli yake yenye utata imezua hasira na kukosolewa na watu wengi, wakati ambapo wafuasi wake wakiwa na hasira wamekataa kukubali uamuzi wa mahakama na walifanya vurugu siku mbili zilizopita. Watatu kati yao walipoteza maisha kutokana na makabiliano na polisi siku ya Ijumaa.

Baada ya kutimuliwa, Park Geun-hye amepoteza kinga yake ya urais. Kuna hatari ya kufunguliwa mashitaka ya jinai kwa rushwa, matumizi mabaya ya madaraka na wizi.