GHANA-SIASA-UCHUMI

Serikali yenye mawaziri 110 yaundwa Ghana

Rais wa Ghana amekosolewa vikali kwa kuteua mawaziri 110 katika serikali yake ikiwa rekodi katika historia ya nchi hiyo. Uchumi wa Ghana unakabiliwa na deni ambalo ni Dola bilioni 30.

Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo, katika hafla ya kuapishwa kwake katika mji wa Accra, Januari 7, 2017.
Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo, katika hafla ya kuapishwa kwake katika mji wa Accra, Januari 7, 2017. REUTERS/Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

Rais Nana Akufo Addo alisema Jumatano wiki hii kuwa aliteuliwa mawaziri 50 na manaibu waziri wanne wa Serikali mpya.

Idadi hiyo imefikia mawaziri 110 kwa jumla katika serikali yake.

Baadhi ya wizara zina karibu mawaziri wanne ikiwa ni pamoja na maafisa wengine.

Mawaziri walioteuliwa watakuwa na haki ya kuwa na magari ya kazi, watakapostaafu na faida nyingine.

Kiongozi wa upinzani, ambao una wajumbe wachache bungeni ameshtumu kile alichokiita "serikali kubwa" ambayoitamaliza rasilimali chache za nchini ya Ghana.

Waziri wa Habari, Mustapha Hamid ametetea uteuzi huo, akisema kuwa rais anawahitaji mawaziri hao walioteuliwa kwa kushughulikia matatizo mengi ya nchi.