UHOLANZI-SIASA-UCHAGUZI

Ulaya yafurahia ushindi wa Mark Rutte nchini Uholanzi

Mark Rutte, kiongozi wa chama vha VVD nchini Uholanzi.
Mark Rutte, kiongozi wa chama vha VVD nchini Uholanzi. Reuters//Toussaint Kluiters/United Photos

Viongozi wa Ulaya wameonyesha Alhamisi wiki hii furaha yao baada ya ushindi katika uchaguzi wa wabunge nchini Uholanzi wa Waziri Mkuu Mark Rutte, ambaye chama chake kitaanza mazungumzo kwa minajili ya kuunda serikali.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na kituo cha utangazaji cha serikali cha NOS, chama cha Liberal Democratic Party (VVD) cha Mark Rutte kiinaongoza, kwa viti 33vya wabunge.

Pamoja na viti 20, chama cha PVV cha Geert Wilders kimepata viti vitano ikilinganishwa na uchaguzi wa mwaka 2012, lakini kimesonga mbele kwa kupata viti vinane ikilinganishwa na bunge linalomaliza muda wake.

Matokeo ya mwanzoni kufuatia uchaguzi wa Uholanzi yanaonyesha chama cha Waziri Mkuu Mark Rutte kimeshinda viti vingi katika bunge.

Chama hicho kimekishinda chama cha kitaifa cha Geert Wilders kilichokuwa dhidi ya wahamiaji na Uislam kwa kura nyingi kuliko ilivyotarajiwa.

Wakati ambapo zaidi ya nusu ya kura zikiwa tayari zimehisabiwa, Kituo cha Rutte cha mrengo wa kulia cha chama cha People’s Party for Freedom and Democracy kinatarajiwa kuchukua viti 32 kati ya 150, kitakacho kuwa kinaongoza kuliko chama chochote kingine.

Vyama vitatu vinatarajiwa kushinda viti 19 kila kimoja, kikiwemo chama cha Wilders’ anti-immigration Freedom Party, na chama cha Christian Democrats na Chama cha D66.

Muundo mpya wa Bunge utatangazwa pamoja na matokeo rasmi Machi 21.

Maafisa wanasema watu wengi walijitokeza kupiga kura zaidi kuliko wakati wowote katika miongo mitatu iliopita, na kufikia asilimia 81.