LEBANON-MAANDAMANO-USALAMA-UCHUMI

Maandamano makubwa dhidi ya kupanda kwa kodi yatokea nchini Lebanon

Beirut, Machi 19, 2017. Maelfu ya waandamanaji walikusanyika nje ya makao makuu ya serikali (kwa nyuma) wakipinga kupanda kwa kodi.
Beirut, Machi 19, 2017. Maelfu ya waandamanaji walikusanyika nje ya makao makuu ya serikali (kwa nyuma) wakipinga kupanda kwa kodi. REUTERS/Alia Haju

Makabiliano makali yalitokea Jumapili hii katika mji wa Beirut kati ya polisi na waandamanaji wakipinga dhidi kupanda kwa kodi na rushwa ambavyo vimeiathiri nchi hiyo. Waziri Mkuu Saad Hariri alikaribishwa kwa kurushiwa chupa zenye maji na marungu alipokua akiwahotubia waandamanaji.

Matangazo ya kibiashara

Maelfu ya raia waliitikia wito wa vyama vya siasa na makundi ya vyama vya kiraia kupinga dhidi ya ongezeko la kodi na ushuru kwa kufadhili muundo mpya wa mshahara katika sekta ya umma na vikosi vya silaha.

waandamanaji walikusanyika katika jiji la Beirut karibu na eno la Grand Serail kunakopatikana ofisi ya Waziri Mkuu.

Askari na polisi walitumwa kuzuia waandamanaji kuendelea kuandamana kuelekea ofisi ya kiongozi wa serikali. Lakini mvutano ulizuka haraka wakati makundi ya vijana walipojaribu kuvuka kwa nguvu vizuizi vya usalama vilivyowekwa na jeshi na polisi, wakati umati wa watu walikua wakiimba nyimbo zinazowashtumu wanasiasa kujihusisha na rushwa.

Waziri Mkuu Saad Hariri alijaribu kutuliza hasira ya waandamanaji, akiwahakikishia kuwa serikali yake itashughulikia madai yao. Lakini hotuba yake ilikatishwa na nyimbo na kutupwa kwa chupa yenye maji na vitu vingine. Aliendelea na hotuba yake na jioni kwenye ukurasa wake wa Twitter aliwataka waandamanaji, kuanzisha "mazungumzo chanya" na serikali.

Hata hivyo, machafuko ya kijamii yanaendelea kuikumba Lebanon na maandamano mengine yamepangwa kufanyika Jumatano Machi 22.