Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa achunguzwa
Imechapishwa:
Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Ufaransa Bruno Le Roux anachunguzwa baada ya madai kuwa, aliwaajiri mabinti wake wawili kama wasaidizi wake alipokuwa mbunge.
Le Roux mwenye umri wa miaka 51, anakutana na Waziri Mkuu Bernard Cazeneuve baadaye sikuy ya Jumanne, kujieleza kuhusu madai haya.
Kituo cha Habari cha TMC, kimeripoti kuwa Le Roux wakati akiwa Mhunge aliwaajiri mabinti wake kati ya mwaka 2009 na 2016 na kuwalipa Dola za Marekani 59,000.
Madai haya yamewakumbusha raia wa Ufaransa kuhusu Francois Fillon mgombea urais nchini humo kupitia chama cha Republican ambaye pia amedaiwa.
Licha ya madai haya, sheria nchini Ufaransa inawaruhusu wabunge kuwaajiri watu wa Familia zao ikiwa watafanya kazi itakayotambuliwa.
Hata hivyo, Fillion na sasa Le Roux kutoka chama cha Kisosholisti wanadaiwa kutoa ajira hizo lakini watu wao wa familia hawakufanya kazi kama ilivyodaiwa.