DRC-UN-SIASA

Wasiwasi juu ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Zinasalia siku nane kabla ya tume ya Umoja wa Mataifa nchini DRC kuongezewa upya muda wa kubaki nchini humo.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Zinasalia siku nane kabla ya tume ya Umoja wa Mataifa nchini DRC kuongezewa upya muda wa kubaki nchini humo. Manuel ELIAS / SC Chamber / AFP

Ikiwa zimesalia siku nane kabla ya tume ya Umoja wa mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (MONUSCO) kuongezewa upya muda wa kubaki nchini humo, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limewasikiliza wadau wakuu katika mgogoro unaoikabili nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Miongoni na wadau hao ni pamoja na, Askafu Utembi, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Maaskofu wa kanisa Katoliki nchini DRC (Cenco) ambaye alionya hatari ya kuahirishwa kwa uchaguzi na kuomba kuimarishwa kwa MONUSCO. Lakini uamuzi wa utawala wa Trump unataka kupunguza bajeti ya matumizi ya kikosi hicho na idadi ya askari. Umoja wa Mataifa nchini DRC unaweza kuwa wa kwanza kulipa gharama zote za matumizi yake.

Kuhusu uhalali, Baraza la Usalama limetamka kwa kauli moja. Ni lazima kuweka kwenye mamlaka ya baadaye ya MONUSCO mkataba wa Desemba 31 mwaka 2016. Askofu Utembi, Mwenyekiti wa Cenco alikwenda kuutetea mbelr ya mabalozi kumi na tano wa Baraza la Usalamla Umoja wa Mataifa. Kuendelea kwa hali hii kunaweza kuuweka hatarini makubaliano ya Desemba 31, 2016 na kutoa fursa kwa uchaguzi wa urais wa Desemba 2017 kuahirishwa na hivyo kupelekea kufanyika kwa kura ya maoni au marekebisho ya katiba. "

"Hatuwezi kucheza na moto"

Lakini ni katika fomu hiyo kumeibuka tofauti na mvutano. Wamarekani wanataka kushughulikia suala la ujumbe wa kulinda amani ulio na gharama mno kwa upande wao. Ufaransa inayoongoza mazungumzo kwa kuiongezea upya MONUSCO muda wa kubaki DRC imetoa ujumbe wa nguvu kwa Marekani: "Hatuwezi kucheza na moto kuhusiana na nchi hii kubwa katika ukanda wa Afrika ya Kati ambapo utulivu ni muhimu kwa nchi hiyo na kwa ukanda wote. "

Maelewano

Katika mapendekezo yake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliomba kudumisha kushikilia kiwango cha sasa cha askari walioko nchini humo na kutuma vitengo viwili vya polisi wa ziada. Maelewano yanaweza kuwa ya kurejelea nafasi ya nafasi ya vikosi visio kuwa kwa kuhakikisha ulinzi wa raia na kufikiria mkakati wa kuindoa MONUSCO kama uchaguzi utafanyika mwezi Desemba 2017.