ARGENTINA-HAKI

Rais wa zamani wa Argentina kusimama kizimbani

Aliyekuwa rais wa Argentina Cristina Fernandez de Kirchner atakiwa kufikishwa mahakamani.
Aliyekuwa rais wa Argentina Cristina Fernandez de Kirchner atakiwa kufikishwa mahakamani. REUTERS/Enrique Garcia Medina

Mahakama nchini Argentina imeagiza kuwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Cristina Fernandez de Kirchner afikishwe mahakamani ili kusikiliza mashtaka dhidi yake ya matumizi mabaya ya fedha.

Matangazo ya kibiashara

Mwendesha mashtaka amesema matumizi mabaya ya fedha ya aliyekuwa rais wa Argentina yameikosesha Argentina mamilioni ya dola.

Fernandez de Kirchner amekanusha kuwa hajafanya makosa kama hayo nakbaini kuwa kesi hiyo ina inaendeshwa kisiasa.

Fernandez ambaye alikuwa rais wa kuanzia mwaka 2007 mpaka mwaka 2015 amekuwa akihusishwa na vitendo vya rushwa.

Fernandez na maafisa wengine 13 akiwemo waziri wa zamani wa uchumi na aliyekuwa Mkuu wa Benki kuu ya Argentina wameshutumiwa, kuiamuru Benki kuuza deni la serikali, ili kulilipa kwa gharama ndogo.