BRAZIL-BIASHARA-UCHUMI

Sekta ya nyama matatani Brazil, Waziri wa Kilimo awahakikishia wanunuzi

Blairo Maggi, ameendelea kuzihakikishia nchi za kigeni kuwa kashfa iliyokumba sekta ya Nyama chini mwake, kuwa bidhaa zake si salama, haina maana
Blairo Maggi, ameendelea kuzihakikishia nchi za kigeni kuwa kashfa iliyokumba sekta ya Nyama chini mwake, kuwa bidhaa zake si salama, haina maana EVARISTO SA / AFP

Sekta ya nyama nchini Brazil ibado iko matatani. Mauzo ya nyama kutoka Brazil kwenda nje yamepigwa marufuku na nchi nyingi. Rais wa Brazil Michel Temer anatazamiwa kukutana na mwenzake wa China kujaribu kuvunja mvutano huo.

Matangazo ya kibiashara

Kwa upande wake Waziri wa Kilimo Blairo Maggi amevishtumu vyombo vya vya habari vya kimataifa kuwa vinakuza habari za uzushi, huku akitetea ubora wa nyama za Brazil.

Blairo Maggi, ameendelea kuzihakikishia nchi za kigeni kuwa kashfa iliyokumba sekta ya Nyama chini mwake, kuwa bidhaa zake si salama, haina maana. Waziri wa Kilimo amewashtumu wafanyabiashara wachache wanaosafirisha bidha hiyo kwenda nchi za nje kuwa hawakuheshimu sheria.

Serikali ya Brazil ina wasiwasi kuwa Marekani, China na nchi za Umoja wa Ulaya zinaweza kupiga marufuku kuingiza nyama kutoka Brazil baada ya shutuma hizo za kushtua zilizojitokeza siku ya Ijumaa wiki iliyopita.

Polisi nchini humo walifanya ukaguzi nchi nzima na kushutumu makampuni ya ufungaji nyama JBS, BRF na makapuni mengine madogo madogo kwa kuuza nyama isiyo salama, kuku na bidhaa nyingine za nyama.

Zaidi ya wafanyakazi 30 wa serikali waliokuwa na jukumu la kukagua vitendo hivyo wanachunguzwa kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Soko la nyama kutoka Brazili lafungwa China

Hata hivyo, wafanyabiashara wakubwa wa nyama za Brazil wameweka sheria ambayo Brazil inaichukulia kama "kinyume cha sheria". Baada ya China, Hong Kong na Umoja wa Ulaya, Afrika Kusini, Misri na Algeria pia wamechukua hatua dhidi ya nyama kutoka Brazil.

Nchi ya China imepiga marufuku kabisa uingizaji wa nyama nyekundu kutoka Brazil, wakati Umoja wa Ulaya ikitangaza kuacha kununua nyama, kuku na bidhaa nyingine kutoka makampuni yaliyohusika na kashfa.

Blairo Maggi amesema kuwa udhibiti wa usafi kwa biashara ya nyama unapewa kipaumbele, huku akiwataka wateja kutokua na hofu ya kula nyama kutoka Brazil.