Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-ZUMA-SIASA

Cyril Ramaphosa: Waandamanaji watakiwa kusikilizwa

Makamu wa rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa awataka viongozi wa Afrika Kusini kusikiliza madai ya waandamanaji.akiwa katika zira ya kikazi China.
Makamu wa rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa awataka viongozi wa Afrika Kusini kusikiliza madai ya waandamanaji.akiwa katika zira ya kikazi China. REUTERS/Siphiwe Sibeko
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 1

Naibu rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amewaambia viongozi wa nchi hiyo kusikiliza waandamanaji, ujumbe ambao umemlenga rais Jacob Zuma. Hata hivyo Zuma ameendelea kusema kuwa maandamano dhidi yake hayana msingi wowote.

Matangazo ya kibiashara

Wito huu umekuja baada ya kuendelea kushuhudiwa kwa maandamano katika miji mbalimbali ya nchini hiyo kushinikiza kujiuzulu kwa rais Zuma, kwa madai ya ufisadi na uongozi mbaya.

Shinikizo hizi zilianza kushuhudiwa mwezi uliopita baada ya Zuma, kulibadilisha baraza la Mawaziri na kumfuta kazi aliyekuwa Waziri wa fedha Pravin Gordhan.

Hatua hii ilimkasirisha Naibu rais Ramaphosa ambaye alisema wazi kuwa hakumuunga mkono rasi Zuma kwa hatua hiyo.

Chama tawala cha ANC kimesema hakina sababu ya kumshinikiza rais Zuma kujiuzulu, huku wabunge wa chama hicho wakionekana kugawanyika.

Zuma mwenyewe amekuwa akisema madai dhidi yake si ya kweli.

Vyama vya upinzani vimeandaa kuwasilisha mswada wa kukosa imani na rais huyo hivi karibuni, kuamua hatima yake bungeni.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.