NIGERIA-UCHUMI

Uwanja wa ndege wa Abuja wafunguliwa baada ya usafiri kusitishwa kwa wiki sita

Uwanja wa kimataifa wa Nnamdi Azikwe,  Abuja, muda mfupi kabla ya kufungwa kwa ajili ya shughuli za ukarabati.
Uwanja wa kimataifa wa Nnamdi Azikwe, Abuja, muda mfupi kabla ya kufungwa kwa ajili ya shughuli za ukarabati. STEFAN HEUNIS / AFP

Baada ya wiki sita ya kufungwa kwa minajili ya kukarabati eneo la ndege zinakotua, uwanja wa ndege wa mji mkuu wa Nigeria, Abuja, umefunguliwa upya siku ya Jumanne, Aprili 18, siku moja kabla ya ratiba rasmi kuanza.

Matangazo ya kibiashara

Eneo hilo lilikarabatiwa kwa ustadi wa hali ya juu. Eneo hilo pia lilikarabatiwa kwa kuweza kupokea wasafiri wenye ulemavu.

Mamlaka ya uwanja wa ndege imeelezea furaha yake. Pia mamlaka ya usafiri wa reli imeelezea furaha yake baada ya kuingiza fedha nyingi kwenye hazina yake kwa muda wote huo wa wiki sita ambapo safari za ndege kati ya Abuja na Kaduna zilikua zimesitishwa.

Waziri wa Uchukuzi, Hadi Sarika alitoa ahadi ya kujiuzulu kama kazi hii ya kukarabati uwanja wa ndege wa Abuja itazidi muda uliopangwa. Afisa huyo amejipongeza. Nafasi yake ya waziri ilikua mashakani. Kufunguliwa upya kwa uwanja huo, saa 24 kabla ya ratiba rasmi kuanza ni habari njema kwa ajili ya biashara mjini Abuja. Kazi za uchukuzi kwa gari ndogo ndogo kama vile teksi na migahawa zilikua zimezorota.

Hii ni habari njema pia kwa serikali ya Nigeria. Lakini yeye vigumu kufunika mchafu-ups unasababishwa na usumbufu wa ndege ya kibiashara kwa wiki sita. Ndge za mashirika ya Air France, British Airways, Lufthansa au South African Airways zilikataa kutua katika uwanja wa ndege wa Kaduna, ispokua ndege za shirika la ndege la Ethiopia Airlines. Na ndege ya kwanza kutua katika uwanja wa ndege wa Abuja baada ya shughuli hizo za ukarabati kumalizika siku ya Jumanne ni ile ya shirika la ndege ya Ethiopia Airlines.