COTE D'IVOIRE-SIASA

Upinzani kuanzisha muungano mpya Cote d'Ivoire

Hadi sasa upinzani nchini Cote d'Ivoire umemua kuchukua msimamo wa kususia uchaguzi
Hadi sasa upinzani nchini Cote d'Ivoire umemua kuchukua msimamo wa kususia uchaguzi fr.zil/CC/Wikimedias Commons

Nchini Cote d'Ivoire, upinzani umeanzisha toka siku ya Alhamisi, Aprili 20, muungano mpya. Vyama vinne pamoja na vyama vingi vya wafanyakazi na mashirika ya kiraia yameunda muungano mpya (ESD) Georges Armand Ouégnin ndiye alituliwa kuwa kiongozi wa muungano huo.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya Muungano wa CNC, na Front du refus, vyama vingine vya upinzani vimeanzisha muungano mpya toka siku Alhamisi, Aprili 20.

Muungano huo unaundwa na vyama vya siasa vinne, RPP, AIRD, UNG na FPI pamoja na vyama vingi vya kiraia, ikiwa ni pamoja na Cojep, SYNAP-CI. Muungano huo mpya unaongozwa na Georges Armand Ouégnin, naibu kiongozi wa chama cha RPP, chama cha Laurent Dona Fologo.

Vyama vinvyunda muungano huu mpya vilisaini mkataba unaozungumzia mambo kumi na mbili ikiwa ni pamoja na maridhiano ya kitaifa,kuachiwa huru kwa wafungwa wa kisiasa, uhuru wa vyombo vya habari, sera ya fedha ya nchi au kesi ya Laurent Gbagbo na Charles Ble Goude ICC .

Baada ya hapo, kiongozi wa ESD, George Armand Ouégnin, katika hotuba yake ya kumaliza kikao hicho, alisisitiza kuhusu mambo matatu ya msingi ambayo ni nguzo kubwa ya muungano huo: kufikia maridhiano ya kweli ya kitaifa, uhuru wa kutoa maoni, udhibiti wa sera ya nchi katika mwaka 2020 kwa njia ya uchaguzi huru, wa makubaliano na wa wazi.