Uchaguzi wa urais kufanyika Jumapili Ufaransa, usalama waimarishwa

Wagombea 11 katika uchaguzi wa urais Alhamisi, Aprili 20, 2017 katika mdahalo wa mwisho wa televiseni.
Imehaririwa: 22/04/2017 - 09:57

Kampeni rasmi za wagombea kumi na moja katika kinyang'anyiro hiki cha urais zilianzia Jumatatu 10 hadi Jumamosi Aprili 15 na Jumatatu 17 hadi Ijumaa Aprili 21.Uchaguzi wa urais nchini Ufaransa umepangwa kufanyika Jumapili Aprili 23. Tayari polisi na askari wametumwa katika maeneo mbalimbali ya nchi kwa minajili ya kuimarisha usalama.Duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais nchini Ufaransa itafanyika Jumapili, Aprili 23.Miongoni mwa wagombea hao ni pamoja na François Fillon, Marine Le Pen, Emmanuel Macron, Jean-Luc Melenchon, Benoit Hamon, Nicolas Dupont-Aignan, François Asselineau, Jean Lassalle, Philippe Poutou, Jacques Cheminade na Nathalie Arthaud.Kura za maoni zinaonesha kuwa uchaguzi wa mwaka huu utakuwa mgumu na wenye ushindani, huku karibu asilimia 30 ya wapiga kura wakiwa hawajaamua mpaka sasa watamchagua nani.