Emmanuel Macron na Le Pen waongoza katika duru ya kwanza

Emmanuel Macron na Marine Le Pen waongoza katika uchaguzi wa urais Ufaransa
Emmanuel Macron na Marine Le Pen waongoza katika uchaguzi wa urais Ufaransa RFI

Emmanuel Macron anaongoza katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais nchini Ufaransa kwa 23.7% ya kura, akifuatiwa na Marine Le Pen kwa 21.7%, kulingana na makadirio ya awali ya mshirika wetu Ipsos.

Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo rais wa Ufaransa François Hollande amepongeza Emmanuel Macron kwa simu.

Kwenye ukurasa wake wa Face book, mgombea wa chama cha France Insoumise Jean-Luc Mélenchon amesema hajasahihisha " matokeo yaliyotangzwa kupitia uchunguzi," akibaini kwamba "matokeo ya miji mikubwa bado hayajajulikana."

Wapiga kura Milioni 47 wanaamua ni nani atakayemrithi rais Francois Hollande ambaye mwaka uliopita, alitangaza kutotetea nafasi yake.
Usalama umeimarishwa kote nchini humo kuhakikisha kuwa zoezi hili linafanyika na kumalizika salama.

Hata hivyo, wachambuzi nchini humo wanasema kuwa Marine Le Pen na Emmanuel Macron huenda wakamaliza katika nafasi ya kwanza na ya pili na kumenyana katika mzunguko wa pili.