UFARANSA-UCHAGUZI-SIASA

Macron na Le Pen kumenyana duru ya pili

Emmanuel Macron na Marine Le Pen kumenyana katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais, Ufaransa
Emmanuel Macron na Marine Le Pen kumenyana katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais, Ufaransa Studio Graphique FMM/AFP

Emmanuel Macron atamenyana na Marine Le Pen katika duru ya pili ya Uchaguzi wa urais nchini Ufaransa tarehe 7 mwezi ujao. Wagombea katika uchaguzi huo wa urais walikua 11.

Matangazo ya kibiashara

Macron alishinda Uchaguzi uliofanyika mwishoni mwa wiki kwa kupata asilimia 23.9 huku Bi. Le Pen akiwa wa pili kwa asilimia 21.4.

Macron mwenye umri wa miaka thelathini na tisa na aliyewahi kuwekeza katika sekta ya benki, hajawahi kuingia katika kinyang'anyiro cha uchaguzi kabla, amesema, shaka, hofu na hamu ya mabadiliko aliyokumbana nayo katika kampeni ndio iliyosababisha wapiga kura kuacha vyama vikuu vya kisiasa ambavyo vimekuwepo uongozini kwa miaka thelathini.

Kwa upande wake, Le Pen ameyaelezea matokeo hayo kuwa ni ya kihistoria. Huku akijiita kuwa yeye ni ndio chaguo la wafaransa na kusema kuwa muda umefika wa kuwabadilisha watu.

Yeyote atakayeshinda duru ya pili atakuwa rais wa nchi hiyo.

Raia wengi wa Ufaransa walijitokeza kupiga kura, katika Uchaguzi uliofanyika chini ya ulinzi.

Wapiga kura Milioni 47 walopiga kura, huku kiwango cha ushiriki kikizidi 60 %.