UFARANSA-MACRON-SIASA

Uchaguzi wa urais Ufaransa: Emmanuel Macron apata 24.01%

Emmanuel Macron atapambana baada ya wiiki mbili katika duru ya pili na Marine le Pen ambae ni mgombea wa chama chenye mrengo wa kulia cha National Front.
Emmanuel Macron atapambana baada ya wiiki mbili katika duru ya pili na Marine le Pen ambae ni mgombea wa chama chenye mrengo wa kulia cha National Front. REUTERS/Philippe Laurenson

Kwa mujibu wa matokeo ya mwisho ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais nchini Ufaransa yaliyotangazwa na Wizara ya Mambo ya Ndani, mgombea wa En Marche! amemshinda Marine Le Pen aliyepata 21.30% ya kura. François Fillon amechukua nafasi ya tatu akipata 20.01%, huku Jean-Luc Mélenchon akichukua nafasi ya kwa 19.58% ya kura.

Matangazo ya kibiashara

Hayo yakijri rais wa Ufaransa François Hollande atangaza kuwa katika duru ya pili atampiga kura Emmanuel Macron

 

Katika hotuba iliyorushwa kwenye televisheni, Rais François Hollande ametoa wito kuzingatia dhidi ya "nchi kuwa hatarini" ambayo itasababishwa na ushindi wa Marine Le Pen katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais. Rais Hollande Ametangaza kwamba atampiga kura mgombea wa En Marche! Emmanuel Macron.
Siku ya Jumapili usiku rais wa Ufaransa François Hollande alimpongeza Emmanuel Macron kwa kupata ushindi dhidi ya mshindani wake Marine Le Pen.

Emmanuel Macron atapambana baada ya wiiki mbili katika duru ya pili na Marine le Pen ambae ni mgombea wa chama chenye mrengo wa kulia cha National Front.

Macron mwenye umri wa miaka thelathini na tisa na aliyewahi kuwekeza katika sekta ya benki, hajawahi kuingia katika kinyang'anyiro cha uchaguzi kabla, amesema, shaka, hofu na hamu ya mabadiliko aliyokumbana nayo katika kampeni ndio iliyosababisha wapiga kura kuacha vyama vikuu vya kisiasa ambavyo vimekuwepo uongozini kwa miaka thelathini.

Matokeo rasmi ya mwisho ya duru ya kwanza.
Matokeo rasmi ya mwisho ya duru ya kwanza. Emmanuelle NICOLAS/FMM