UFARANSA-MACRON-LE PEN-SIASA

Macron na Le Pen warushiana vijembe Whirlpool

Emmanuel Macron akizungukwa na waandishi wa habari alipowasili katika kiwanda cha Whirlpool katika mji wa Amiens Jumatano hii Aprili 26, 2017.
Emmanuel Macron akizungukwa na waandishi wa habari alipowasili katika kiwanda cha Whirlpool katika mji wa Amiens Jumatano hii Aprili 26, 2017. REUTERS/Pascal Rossignol

Kampeni ya duru ya pili ya uchaguzi wa urais imeendelea kwa kasi siku ya Jumatano kwa ziara ghafla ya Marine Le Pen katika eneo la Whirlpool katika mji wa Amiens ambapo Emmanuel Macron, alizuru muda mfupi baadaye, alipokelea na umati wa watu kabla ya kuzungumza na wafanyakazi. Hali hii ilizua mgongano katika kampeni hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatano mchana Marine Le Pen alitembelea kiwanda cha Whirlpool ambacho aliahidi kukifunga, wakati ambapo, kwenye umbali wa kilomita chache tu, Emmanuel Macron alikua akikutana kwa mazungumzo na wawakilishi wa chama cha wafanyakazi wa kiwanda hicho.

"Mimi niko pamoja na wafanyakazi kwenye sehemu ya kuegesha magari, si katika migahawa ya Amiens," Marine Le Pen aliambia vyombo vya habari. Marine Le Pen alipigwa picha kwa zaidi ya dakika kumi akiwa pamoja na wafanyakazi, huku wengine wakitokwa machozi, na kujipiga picha kweye simu zao.

Mgombea wa En Marche! alijibu mashambulizi hayo, akitangaza kuwatembelea mchana wafanyakazi wa kampuni ya Whirlpool, akiambatana na wawakilishi wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi. "Bi Le Pen anatumia watu kiiasa, kwa kuwadanganya kwenye eneo la kuegeshea magari," Bw Macron alijibu.

Usiku, Emmanuel Macron anatazamiwa kufanya mkutano wa hadhara katika mji wa Arras.