UFARANSA-UCHAGUZI

Macron na Le Pen warudi uwanjani kunadi sera zao

Emmanuel Macron na Le Pen, Aprili 23, 2017.
Emmanuel Macron na Le Pen, Aprili 23, 2017. Eric Feferberg, Joël SAGET / AFP

Wiki moja kabla ya mwisho wa kampeni rasmi kwa ajili ya duru ya pili ya uchaguzi wa urais, Marine Le Pen na Emmanuel Macron wanaendelea kupambana katika kampeni na midahalo ya televisheni. Chama cha FN, ambacho kinajaribu pia kuhamasisha wapiga kura wa mrengo wa kulia, kinashtumiwa kuwa chama cha "kibaguzi".

Matangazo ya kibiashara

"Ni kwa bahati mbaya," amekiri Marine Le Pen kama alichagua mkoa wa Nice kuwa mkoa wa kwanza kuanza kuzuru katika kampeni yake ya duru ya pili ya uchaguzi wa urais. Nice ambayo Wagiriki wanaita Nikaia, ikimaanisha, "pale ambapo ushindi ulitokea." Hata kama Le Pen anaendelea na kampeni yake, anaamini kwamba ataweza kumuangusha Emmanuel Macron ambaye anajaribu "kutumia jina la wazalendo" , amesema Bi Le Pen. Katika hali ya kurushiana vijembe na kauli zenye chuki, Marine Le Pen amesema yeye yuko kama "David akipambana dhidi ya Goliathi," akitoa wito wa "kuwapiku" wapinzani wake,akiwapuzia wanasiasa vigogo wanaomuunga mkono Emmanuel Macron kama Robert Hue, Manuel Valls na hasa Christian Estrosi, Rais wa mkoa wa Provence-Alpes-Côte d'Azur, ambaye kwa muda mrefu alizomelewa na wafuasi 4000 wa chama cha FN.

Wakati huo huo Emmanuel Macron aliendelea na kampeni yake katika mji wa Sarcelles, karibu na mji wa Paris, katika mji muhimu ambapo alikutana na wanaharakati wa mashirika mbalimbali na vijana, ambapo kwa muda wa dakika kadhaa alicheza mpira wa miguu, na alimshambuliwa Le Pen, huku akipuuzia na kulaani chama cha FN cha marine Le Pen akisema kuwa ni "chama cha kibaguzi, ambacho kinawakilishwa katika uchaguzi wa urais na mtu mwenye misimamo ya ajabu".

Baada ya kuzu eneo moja la mji wa Ufaransa, Emmanuel Macron alishiriki mdahalo wa televisheni ya TFI. Ili kujibu wale wanaomshtumu kutangaza ushindi, Bw Macron hakuweza kuvumilia lugha hizo akisem akuwa ni lugha potovu.