Jean-Marie na Marine Le Pen wamshambulia Emmanuel Macron
Imechapishwa:
Katika mkutano wa kampeni yake alioendesha mjini mjini Paris, Marine Le Pen, mgombea katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais nchini Ufaransa amemshambulia vikali Emmanuel Macron, ambaye pia ni mogmbea katika uchaguzi huo.
Kiongozi wa chama cha FN, alijiunga na Nicolas Dupont Aignan aliyemuahidi kumteua kuwa waziri wake mkuu, kwa kumshambulia mpinzani wake katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais unaopangwa kufanyika tarehe 7 Mei, 2017.
Mgombea wa mrengo wa kulia alitangaza siku ya Jumatatu alitoa maneno makalidhidi ya mpinzani wake Emmanuel Macron.
Marine Le Pen katika eneo la maonyesho la Villepinte, alisema kuwa adui yake ni fedha akimfananisha Emmanuel Macron na François Hollande.
"Adui yetu ni fedha. Lakini wakati huu mpinzani wetu, ana jina, ana uso. Ni Emmanuel Macron ", amesema Marine Le Pen mbele ya wafuasi wake waliokua walikusanyika katia eneo la maonyesho la Villepinte. Kwa mujibu wa Le Pen, Emmanuel Macron, ni François Hollande, ambaye anataka kusalia madarakani kwa nguvu. "Naam mgombea huyo anayemaliza muda wake, tutamuondoa! ", Le Pen ameahidi.
Bi Le Pen alitoa hotuba yake hiyo mbele ya wanasiasa vigogo walioungana naye hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na Florian Philippot, Marion Maréchal-Le Pen, Louis Aliot, David Rachline, meya wa mji wa Béziers Robert Ménard, bila kusahau mshirika mpya wa Marine Le Pen, Nicolas Dupont-Aignan, ambaye alifungua mkutano wa kampeni hiyo kwa kusema: ". Tuna miadi na historia kubwa ya Ufaransa".