Wafuasi wengi wa Jean-Luc Mélenchon wakataa kuonyesha msimamo wao
Imechapishwa:
Kwa mujibu wa matokeo ya mashauriano kwenye Intaneti, 65% ya wafuasi wa chama cha France Insoumise cha Jean-Luc Mélenchon wanatazamiwa kupiga kura, au kuacha kupiga kura katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais ambapo Emmanuel Macron atapambana Jumapili Mei 7 na Marine Le Pen.
Kwa mujibu wa mashauriano yaliyorushwa kwenye intaneti, 36% ya wapiga kura takriban 243,000 wamechagua kupiga kura bila hata hivyo kubaini mtu watakaye mpigia kura na 29% kuacha kupiga katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais siku ya Jumapili. % 35 tu wamekubali kumpigia kura Emmanuel Macron.
Mgombea wa caham cah France Insoumise Jean-Luc Mélenchon, ambaye alipata 19.5% ya kura katika duru ya kwanza, alitangaza kutompigia kura Marine Le Pen, lakini bado hadi sasa hajawatolea wito wafuasi wake kumpigia kura Emmanuel Macron.
Jean-Luc Mélenchon alieleza kwamba mashauriano haya yaliofanywa kwa takriban watu 430,000 walioprodheshwa kwenye intaneti hayakua yamelenga "kuamua kupiga kura kwa maelekezo" lakini kuruhusu wafuasi wake kutoa uamuzi wao kwa duru ya pili.
Chaguo ambalo msemaji wa serikali Stéphane Le Foll ameita "kosa.