UFARANSA-MACRON-SIASA

Emmanuel Macron rais wa nane wa awamu ya tano nchini Ufaransa

Emmanuel Macron jioni ya duru ya 1 ya uchaguzi wa urais
Emmanuel Macron jioni ya duru ya 1 ya uchaguzi wa urais REUTERS/Benoit Tessier/File Photo

Emmanul Macron ambaye hakujulikana katika siasa miaka na kabla ya miezi kumi tatu ya uchaguzi wa urais haukua na chama chochote, alichaguliwa Jumapili hii Mei 7 rais wa nane wa awamu ya tanu akiwa na miaka 39.

Matangazo ya kibiashara

Emmanuel Macron aliibuka mshindi dhidi ya mpinzani wake Marine Le Pen katika duru ya pili kwa 66.06% ya kura.

Emmanuel Macron ni rais ambaye bado kijana wa awamu ya tanu ya jamhuri ya Ufaransa.

 Katika taarifa yake, Emmanuel Macron alisema kwamba Ufaransa imefanikiwa kufungua ukurasa mpya katika historia yake na kwamba alikuwa na ndoto ya kuwa mpiga mbiu wa nchi hiyo kwa kugunduliwa upya kwa matumaini na imani.Mshndi huyo wa nafasi ya urais ametoa hotuba yale ya kwanza akiwa ni raisi mteule. Emmanuel Macron, amenukuliwa akisema kwamba atahakikiksha anafanya kila linalowezekana kulipa fadhila ya uaminifu wa wafaransa waliompa.

Macron pia alitoa shukrani kwa wapiga kura ambao hawakumpigia kura akisema wametekeleza haki yao ya msingi ya kuchagua kiongozi waliyemtaka ambapo amesema licha ya yote hayo bado anawaona ni raia wa Ufaransa na wanastahili kusikilizwa.

Wafaransa wenzangu, mlioko ndani na nje ya ufaransa, baada ya vita ya muda mrefu vya kidemokrasia , na kuchagua kuweka imani yenu juu yangu. Ningependa kuchukua fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa heshima kubwa.

Macron alisema jukumu lililoko mbele yake ni kuhakikisha analinda maslahi ya taifa ya Ufaransa kwenye umoja wa Ulaya na kwamba kama alivyoahidi wakati wa kampeni anataka kuona Ulaya mpya chini ya uongozi wake.

Kuhusu huduma za kijamii Macron alisema anatambua changamoto za kijamii zilizoko ikiwa ni pamoja na hali tete ya uchumi na tatizo la ukosefu wa ajira nchini matatizo aliyosema anatambua namna ambavyo wananchi wamechoshwa na hali ya mambo ilivyo.

Muda mfupi uliopita Marine Le Pen aliwahutubia wafuasi wake na kutangaza kumpongeza Macron kwa ushindi alioupata huku akisema uchaguzi huu umekuwa ni wa kihistoria.

Le Pen alisema matokeo haya yametoa taswira mpya kwa siasa za Ufaransa ambapo amewashukuru wapiga kura wake kwa kumuunga mkono toka kwenye duru ya kwanza ya uchaguzi.

Kiongozi huyo ameongeza kuwa yeye ataongoza upinzani bungeni ili katika kuhakikisha nchi yao inarejea kwenye ramani ya dunia.