DRC-SIASA

Serikali mpya DRC yatangazwa lakini hakuna mabadiliko makubwa

Waziri Mkuu Bruno Tshibala, kabla ya uteuzi wake Aprili 4, 2017, Kinshasa.
Waziri Mkuu Bruno Tshibala, kabla ya uteuzi wake Aprili 4, 2017, Kinshasa. JUNIOR KANNAH / AFP

Nchini DRC, karibu mwezi mmoja baada ya uteuzi wa Waziri Mkuu Bruno Tshibala, serikali mpya ilitangazwa siku ya Jumanne, Mei 9. Hakuna mabadiliko kwenye nyadhifa muhimu.

Matangazo ya kibiashara

Wanasiasa muhimu wa upinzani waliojiondoa kwenye muungano wao wa upinzani waliteuliwa katika serikali hiyo mpya, licha wanasiasa vigogo wa upinzani kuendelea kuipinga.

Nafasi muhimu kama vile wizara ya Mambo ya Ndani, wizara Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje, wizara ya Ulinzi, wizara ya Madini na Mafuta, zimeendelea kushikiliwa na mawaziri walioteuliwa mwezi Desemba 2016 ambao karibu wote ni kutoka chama tawala cha PPRD na washirika wa karibu wa rais Joseph Kabila.

Msemaji wa Serikali na Waziri wa Mawasiliano pia hakubadilishwa na fasi yake ni Lambert Mende.

Wanasiasa wa upinzani waliojiondoa kwenye muungano wao wa upinzani na kukubali kumfuata Waziri Mkuu Bruno Tshibala, ambao ni makada wa zamani wa chama kikuu cha upinzani cha UDPS waliokubali kuungana na utawala. Jean-Pierre Lisanga Bonganga, wa muungano wa washirika wa Etienne Tshisekedi, aliteuliwa Waziri wa Mahusiano na Bunge.

Waziri mpya wa Posta na Mawasiliano ni Emery Okundji, pia kutoka upinzani, pamoja na Waziri wa Ardhi, Lumeya Dhu Maleghi, bila kusahau Freddy Kita, mshirika wa karibu wa zamani wa mpinzani Eugène Diomi Ndongala, aliteuliwa Naibu Waziri wa Ushirikiano.

Hata hivyo, baadhi ya wanasiasa wanaodaiwa kuwa washirika wa karibu wa Bruno Tshibala hawakuteuliwa katika serikali hiyo mpya, miongoni mwao ni pamoja na Joseph Oleghankoy au ndugu wa kambo wa mpinzani Moise Katumbi, Raphael Katebe Katoto.

Idadi ya mawaziri ilipunguzwa kutoa mawaziri 67 hadi 58, lakini bado ina tatizo kama lile la serikali iliyoyotangulia ya kutambuliwa na upinzani. serikali hiyo iliundwa kinyume na makubaliano yaliyoafikiwa kati ya serikali na upinzani Desemba 31, 2017, kwa mujibu wa wanasiasa vigogo wa upinzani waliokataa kujiunga na utawala.