IRELAND-SIASA

Waziri Mkuu wa Ireland atangaza kujiuzulu

Waziri Mkuu wa Ireland Enda Kenny atangaza kuachia ngazi.
Waziri Mkuu wa Ireland Enda Kenny atangaza kuachia ngazi. REUTERS/Francois Lenoir

Siku ya Jumatano Mei 17 Waziri Mkuu wa Ireland Enda Kenny alitangaza kujiuzulu kwenye uongozi wa chama chake cha mrengo wa kulia cha Fine Gael. Wakati huo huo ametangaza kuachia ngazi kwenye nafasi ya waziri mkuu.

Matangazo ya kibiashara

Enda Kenny alikuwa alitangaza kuondoka kwenye nafasi hiyo kwa muda mrefu. Enda Kenny alikua kiongozi wa chama Fine Gael kwa muda wa miaka 15 ambapo chama chake kilishinda uchaguzi mkuu mara mbili na baada ya miaka sita madarakani alitaka kukabidhi madaraka, lakini matukio kadhaa yamesababisha kuharakisha kuondoka kwake.

Enda Kenny ataendelea kuhudumu kama waziri mkuu hadi Juni 2, wakati wa kumchagua mrithi wake kwenye uongozi wa chama na kwenye nafasi ya waziri mkuu, lakini siku ya Jumatano.

Enda Kenny kiongozi wa kwanza wa chama cha Fine Gael alishinda uchaguzi mkuu mara mbili mfululizo na alirithi mwaka jana serikali ya kwanza ya wachache katika historia ya Ireland. Ingawa usimamizi wake katika mgogoro wa fedha uliiondoa nchi yake katika hali hiyo, amekua akikosolewa na kupingwa kutokana na ukosefu wake wa maono, na uongoziwake unakabiliwa na hali ya sintofahamu.

Kutokana na hali hiyo Waziri Mkuu Enda Kenny ametangaza kwamba anaachia ngazi kabla ya kumalizika kwa muhula wake ili kupunguza hasira za wananchi.

Tangu mwanzoni mwa mwaka huu serikali imeendelea kukabiliwa na hali ngumu, ikiwa ni pamoja na kashfa mbalimbali katika polisi, mawasiliano mabovu katika masuala ya biashara na kuongezeka kwa migomo katika sekta ya umma. Enda Kenny anaona ni vizuri kuchukua haraka uamuzi, lakini amekua akiahirisha utekelezaji wa uamuzi wake.

Hatimaye, Enda Kenny amechukua uamuzi huo kutokana na tishio la kupiga kura ya kutokuwa na imani naye bungeni na vita ya ambayo vinaendelea kuhusu atakayemrithi kwenye wadhifa huo.