IRAN-UCHAGUZI-SIASA

Wairani kumchagua rais wao mpya Ijumaa hii

Wafuasi wa rais wa sasa Hassan Rohani wakati wa mkutano wa kampeni siku moja kabla ya uchaguzi, Mei 18 katika Tehran.
Wafuasi wa rais wa sasa Hassan Rohani wakati wa mkutano wa kampeni siku moja kabla ya uchaguzi, Mei 18 katika Tehran. TIMA via REUTERS

Wapiga kura milioni 56.4 walioorodheshwa nchini Iran wanapiga kura Ijumaa hii Mei 19 kumchagua rais wao mpya. Rais anayemaliza muda wake Hassan Rohani, anapewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huo lakini chama chake kimejidhatiti vilivyo baada ya meya wa Tehran na Mwanasheria wa zamani Ebrahim Raissi kujiunga na kambi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Vituo vya kupigia kuravimefunguliwa saa 8:00 asubuhi saa za Tehran. Vituo vya mwishi vitafunga saa 10 jioni. Kwnye kituo cha televisheni ya taifa, Kiongozi Mkuu, Ayatollah Ali Khamenei, alitoa wito kwa raia kuitikia uchaguzi huo.

Wanasiasa kadhaa tayari wamebaini katika vituo ambapo watapigia kura. Rais wa zamani Khatami amesema atakupiga kura "mapema asubuhi" katika eneo la Jamaran, kaskazini mwa mji mkuu. Mmoja wa wagombea wanne, Mostafa Hashemitaba atapiga kura saa 8:30 mashariki ya mji mkuu.

Huu ni uchaguzi wa 12 wa urais nchini humo, utawashirikisha pia wapiga kura wengine Milioni 2.5 watakaopiga kura katika mataifa 103 ikiwa ni pamoja na Marekani.

Ni uchaguzi unaoangaziwa kwa karibu sana na wachambuzi wa siasa katika eneo la Mashariki ya Kati na Mataifa ya Magharibi ambayo kwa muda mrefu  yamekuwa na uhusiano mgumu kutokana na mradi wa Nyuklia wa Iran.

Iran ni taifa lenye nguvu katika eneo la Mashariki ya Kati, na udhabiti wake wa kisiasa utaathiri hatima ya kisiasa ya nchi jirani kama Syria, Yemen na Iraq ambayo yameendelea kukabiliana na changamoto za kiusalama.

Rais Hassan Rouhani ambaye aliingia madarakani mwaka 2013 akiwa na ajenda ya mabadiliko, alifanikiwa kufikia mwafaka kuhusu mradi wa Nyuklia, atamenyana na wagombea wengine watatu.

Wagombea hao ni pamoja na Ebrahim Raisi, Mostafa Mir-Salom na Mostafa Hashemitaba.