MAREKANI-TRUMP-SIASA

Mkuu wa mawasiliano White House ajiuzulu

Rais wa Marekani Donald Trump pata pigi jingine baada ya Mkurugenzi wa mawasiliano katika ikulu ya White House, Mike Dubke, kuachia ngazi.
Rais wa Marekani Donald Trump pata pigi jingine baada ya Mkurugenzi wa mawasiliano katika ikulu ya White House, Mike Dubke, kuachia ngazi. REUTERS/Carlos Barria

Mkurugenzi wa mawasiliano katika ikulu ya White House, Mike Dubke, amejiuzulu miezi mitatu baada ya kutuliwa na Donald Trump kushikilia nafasi hiyo. Uamuzi huo unatokea huku kukiwa na taarifa kwamba kuna migawanyiko katika kundi la maafisa wa mawasiliano katika ikulu ya White House.

Matangazo ya kibiashara

Bw Dubke ameondoka kwa nia njema, kwa mujibu wa tovuti ya kisiasa ya Axios News ambayo ilikuwa ya kwanza kutangaza habari hizo.

Mshauri wa White House Kellyanne Conway amesema kuwa Bw Dubke alikuwa amekubali kusalia kazini hadi Bw Trump arejee kutoka safari yake ya kwanza nje ya nchi hiyo Mashariki ya Kati na Ulaya siku ya Jumamosi.

Mike Dubke, alipewa kazi mwezi Machi kujaribu kufanyia mageuzi mkakati wa mawasiliano wa ikulu ya White House.

Kama sehemu ya mabadiliko aliyopendekeza, afisa wa habari wa White House Sean Spicer ataendelea kushikilia wadhifa wake, lakini vikao vya maafisa hao na wanahabari vitakuwa vichache.

Utawala wa Donald Trump umeendelea kuingiliwa na hali ya sintofahamu na kusababidsha baadhi ya maafisa kuachia ngazi.