Ferrand akataa kujiuzulu, Macron na serikali wamtetea
Hali ya sintofahamu yaendelea kujitokeza nchini Ufaransa, baada ya gazeti la kila wiki la Canard Enchaine kuweka wazi ya operesheni za mali ya Richard Ferrand, ambae ni Waziri wa Mshikamano wa Kitaifa wa Ufaransa.
Imechapishwa:
Alipoulizwa siku ya Jumatano, May 31 kwenye kituo cha habari cha Ufaransa Inter, Richard Ferrand amefutilia mbali hoja ya kujiuzulu. Wakati huo huo rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametolea wito serikali kuwa na "mshikamano", pia akisema kuwa vyombo vya habari (havipaswi kuwa hakimu".
Katika vyama vya mrengo wa kulia na kushoto, wapinzani wa vuguvugu la Republique En Marche (LREM) wanamlenga Waziri wa Mshikamano wa Kitaifa.
Richard Ferrand ameapa kuwa hawezi kujuzulu. "Ndiyo, mimi ni mkweli," Bw Ferrand amesema, wiki moja baada ya ripoti ya kwanza kuhusu shughuli za mali yakampuni ya Mutuelle de Bretagne, ambapo alikuwa Mkurugenzi, na alimshirikisha mpenzi wake.
"Ninajiamini. Sijpakutwa na hatia na Mahakama ya Jamhuri, ambayo ninaheshimu. Ninaelewa kwamba, kidogo kidogo, tuhuma hizi litengenezwa, na tuhuma, ni sumu; tuhuma, ni sumu kwa demokrasia; na ni kawaida kwamba wananchi wa Ufaransa wanajiuliza. "
Chochote kile nilichofanya katika utendaji wangu wa kazi ni halalina kilithibitishwa na bodi ya uongozi ambayo pia iliniunga mkono. Nilionyesha nyaraka zote. Nilitoa mambo yote, kwa hiyo sina hatia," amesema Richard Ferrand.