BRAZIL-SIASA-UCHUMI-HAKI

Rais wa Brazil kujibu tuhuma za rushwa zinazomkabili

Rais wa Brazil, Michel Temer aapa kuwa hatoachia ngazi.
Rais wa Brazil, Michel Temer aapa kuwa hatoachia ngazi. REUTERS/Adriano Machado

Rais wa Brazil Michel Temer amepewa saa 24 kuijibu polisi tuhuma za rushwa zinazomkabili. Hayo yanajiri wakati ambapo maandamano yakiendelea kuikumba miji mbalimbali ya nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Agizo hilo lilitolewa na Mahakama kuu nchini Brazil.

Wadadisi wanasema agizo hili la mahakama kuu linatishia maisha ya kisiasa ya rais Michel Temer.

Rais Michel Temer anatuhumiwa kupokea kiasi kikubwa cha fedha kama rushwa kutoka kwa kampuni kubwa ya usindikaji nyama ,JBS.

Hata hivyo rais Michel Temer amefutilia mbali tuhuma hizo na kusem akuwa ni mpango wa kutaka kumuangusha na ameapa kuwa hatojiuzulu.

Hayo yanajiri wakati ambapo vijana na wanasiasa mbalimbali wanaendelea kuandamana katika miji mbalimbali wakimtaka rais Michel Temer ajiuzulu.