DRC-SIASA

Joseph Kabila: Sijawahi kuahidi kuandaa uchaguzi DR Congo

Rais wa DRC, Joseph Kabila.
Rais wa DRC, Joseph Kabila. REUTERS/Kenny Katombe

Rais wa Jamhuri ya Kidemokradia ya Congo, Joseph Kabila Kabange amesema hajawahi kuahidi kuandaa Uchaguzi Mkuu nchini mwake mwaka huu. 

Matangazo ya kibiashara

Kabila ameliambia Jarida la kila wiki la Ujerumani la Der Spiegel kuwa hajaahidi chochote lakini anapenda Uchaguzi ufanyike haraka iwezekanavyo.

Aidha, amesema anataka uchaguzi mzuri lakini sio tu kufanya uchaguzi.

Hayo yanajiri wakati ambapo joto la kisiasa kuhuu uchaguzi kufanyika mwaka huu nchini DR Congo imeendelea kupanda, huku upinzani hasa ule unaoongozwa na mwana wa aliyekuwa kiongozi wa kihistoria wa upinzani Etienne Tshisekedi ukiendelea kugawanyika.

Hivi karibuni muungano huo wa Rassemblement uligawanyka baada ya uteuzi wa Waziri Mkuu kutoka muungano huo Bruno Tshibala.

Hali ya kisiasa nchini Dr Congo inaendelea kutisha , huko watu wengi wakiendelea kukamatwa na wengine kuuawa.

Wiki iliopita Umoja wa Ulaya na Marekani waliwachukulia vikwazo maafisa kadhaa wa serikali ya DRC kwa kuchochea uhasama na kuchangia kushindwa kuandaa uchaguzi mwaka huu.