AFRIKA KUSINI-ZUMA-UCHUMI

Zuma aendelea kushtumiwa kwa ufisadi

Le président sud-africain Jacob Zuma dément posséder un «palace» aux Emirats arabes unis,
Le président sud-africain Jacob Zuma dément posséder un «palace» aux Emirats arabes unis, REUTERS/Mike Hutchings

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma anaendelea kushtumiwa na kuhusika na vitendo vya ufisadi, huku upinzani na baadhi ya wafuasi vigogo wa chama cha ANC wakimtaka ajiuzulu haraka.

Matangazo ya kibiashara

Mbali na makazi ya kifahari ya Zuma ya Nkandla, siku ya Jumapili Juni 4 gazeti la Afrika Kusini la Sunday Times liliweka wazi ripoti kuhusu uchunguzi waandishi wake waliofanya mjini Dubai mwaka jana kuhusu makazi ya kifahari ya Jacob Zuma yanayopatikana katika mtaa wa Lailak katika eneo la Emirates Hills.

 

Inaarifiwa kuwa nyumba hii ilinunuliwa na familia ya Gupta kwa kitita cha Euro milioni 23 mwaka 2015. Mwaka huo huo, mtoto wa Jacob Zuma, Duduzane, msihirika wa familia ya Gupta, alinunua nyumba ghorofa ya kifahari kwa Euro milioni 1.3 katika eneo maarufu la Burj Khalifa, jengo refu zaidi duniani.

Katika barua pepe zilizogunduliwa wiki iliyopita, kulipatikana barua kadhaa zilizosainiwa na rais Jacob Zuma, ambazo zinazungumzia mradi wa kujenga yake ya pili ya kifahari katika mji wa Dubai.

Rais Jacob Zuma ameendelea kukumbwa na shutma mbalimbali za ufisadi, huku upinzani na mashirika ya kiraia yakimtaka ajiuzulu.

 

Hayo yakijiri Tume ya kupambana na ufisadi nchini Afrika Kusini, inachunguza hatua ya serikali kumpa ulinzi aliyekuwa Mkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika Nkosazana Dlamini-Zuma.

Hatua hii imekuja baada ya kuwepo kwa madai kuwa mke huyo wa zamani wa rais Jacob Zuma huenda akateuliwa na chaa cha ANC kumrithi kiongozi wa sasa.

Vyama vya upinzani nchini humo, kikiongozwa na DA kimekuwa kikilalamika kuwa, Bi.Zuma anaedelea kupokea ulinzi wa serikali ilahali hahudumu katika Ofisi yoyote ya umma.