URUSI-MAANDAMANO-UFISADI

Alexei Navalny ahukumiwa kifungo cha siku 30 jela Urusi

Katika mji wa Moscow, maelfu ya wafuasi wa kiongozi wa upinzani Alexei Navalny, ikiwa ni pamoja na vijana wengi na wanafunzi, walikusanyika kwenye umbali wa mita kadhaa na ikulu ya Kremlin, angalau watu 400 walikamatwa.
Katika mji wa Moscow, maelfu ya wafuasi wa kiongozi wa upinzani Alexei Navalny, ikiwa ni pamoja na vijana wengi na wanafunzi, walikusanyika kwenye umbali wa mita kadhaa na ikulu ya Kremlin, angalau watu 400 walikamatwa. REUTERS/Maxim Shemetov

Kiongozi wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny alikamatwa Jumatatu na wafuasi wake wengi na amehukumia kifungo cha siku 30 jela kwa kukiuka sheria baada ya kuandaa maandamano ya kushtumu viongozi wanaojihusisha na ufisadi.

Matangazo ya kibiashara

Watu kadhaa walikamatwa siku ya Jumatatu Juni 12 katika miji ya Moscow, St Petersburg na miji mingine. Watu hawa waliamatwa wakati wa maandamano ambayo hayakuruhusiwa yaliofanyika kwa wito wa kiongozi wa upinzani Alexei Navalny kwa minajili ya kukemea ufisadi unaoendeshwa na viongozi wa ngazi ya juu serikalini. Bw Navalny alikamatwa kabla ya mkutano wa hadhara.Alifikishwa mchana mahakamani mjini Moscow na alihukumiwa kifungo cha siku 30 kwa kukataa kutii amri ya polisi na kukiuka sheria baada ya kuandaa maandamano.

Waandamanaji, wengi wao wakiwa vijana walilaani tabia za baadhi ya viongozi tawala wanaojihusisha na ufisadi.
Waandamanaji, wengi wao wakiwa vijana walilaani tabia za baadhi ya viongozi tawala wanaojihusisha na ufisadi. REUTERS/Maxim Shemetov

Navalny alikamatwa nyumbani kwake mjini Moscow siku ya Jumatatu kabla ya kufanyika kwa maandamano ya kupinga ufisadi nchini Urusi, lakini kukamatwa kwake hakujakataza wafuasi wake kuingia mitaani.

Waandamanaji, wengi wao wakiwa vijana walilaani tabia za baadhi ya viongozi tawala wanaojihusisha na ufisadi. Moja ya kauli mbiu yao, "Tunapenda Urusi, lakini tumechoshwa na utawala." kauli mbiu nyingine iliokua ikitolewa na umati wa waandamanaji ilikua: ". Moja, mbili, tatu Putin achia ngazi"

Polisi waliwasili kwa wingi na kujitahidi kuzima maandamano yaliokua yakiendelea.

Mahakama ya Moscow iltangaza umuzi wake jana Jumatatu na kukataa wito wa mawakili wa Navalny kufuta kesi hiyo.

Kiongozi huyo wa upinzani mwenye umri wa miaka 42 baadaye alithibitisha hukumu yake katika mtandao wa twitter.