UFARANSA-SIASA

Bayrou na Sarnez wajiuzulu serikalini

Waziri wa Sheria wa Ufaransa François Bayrou atafanya mkutanao na waandishi wa habari Jumatano hii, 21 Juni saa 11:00 jioni.
Waziri wa Sheria wa Ufaransa François Bayrou atafanya mkutanao na waandishi wa habari Jumatano hii, 21 Juni saa 11:00 jioni. RFI/Edmond Sadaka

Waziri wa Sheria wa Ufaransa François Bayrou, mshirika muhimu wa rais Emmanuel Macron, ametangaza Jumatano hii Juni 21 kwenye shirika la habari la AFP kwamba anajiuzulu kwenye wadhifa wake serikalini. Waziri wa Mambo ya Ulaya, Marielle de Sarnez, pia ametangaza kujiuzulu.

Matangazo ya kibiashara

"Nimechukua uamuzi wa kutokua katika serikali ijayo. Nitakua na mkutano na waandishi wa habari saa 11:00 jioni, "amesemakiongozi wa chama cha MoDem, chaa cha mrengo wa kati kinachokabiliwa na uchunguzi juu ya ajira ya wasaidizi wake katika Bunge la Ulaya.

Msemaji wa serikali Christophe Castaner amesema leo asubuhi kwenye kituo cha habari cha Europe 1 "uamuzi binafsi," uamuzi ambao"unapunguza hali inayojiri." "Anataka kujitetea," amesema Christophe Castaner.

Waziri wa Mambo ya Ulaya, Marielle de Sarnez, pia amejuzulu kwenye wadhifa wake serikalini na ataongoza kundi la wabunge 42 kutoka chama cha MoDem Bungeni, chanzo kutoka chama cha MoDem kimetanga Jumatano hii asubuhi kwenye shirika la habari la AFP.

Kufuatia kuondoka kwa Goulard

Mawaziri hawa wawili wanachukua uamuzi huo baada ya Waziri wa Majeshi Sylvie Goulad kujiuzulu tangu siku ya Jumanne.

Mawaziri watatu kutoka chama cha MoDem wamejuzulu kwenye nyadhifa zao serikalini wakati ambapo chama hiki kinakabiliwa na uchunguzi kuhusu ajira ya wasaidizi wake katika Bunge la Ulaya.

Chama cah Republique en Marche cha Emmanuel Macron, kina wabunge wengi Bungeni kikiwa na viti 308.