MAREKANI-UCHAGUZI

Chama cha Republican chashinda katika uchaguzi mdogo wa bunge la Congress

Mgombea wa chama cha Republican Karen Handel akiherehekea ushindi wake dhidi ya Jon Ossoff kutoka chama cha Democratic, Juni 20,2017 Atlanta.
Mgombea wa chama cha Republican Karen Handel akiherehekea ushindi wake dhidi ya Jon Ossoff kutoka chama cha Democratic, Juni 20,2017 Atlanta. REUTERS/Bita Honarvar

Wagombea wa Trump kutoka chama cha Republican wameshinda katika uchaguzi mdogo wa bunge la Congress katika jimbo la Georgia. Uchaguzi huu muhimu ulionekana na wengi kuwa kura ya maoni dhidi ya utawala wa Donald Trump ambaye sheria zake zimekua zikikosolewa na upinzani pamoja na baadhi ya vigogo wa chama chake.

Matangazo ya kibiashara

Chama cha Democratic walitumai kutumia fursa ya kushuka kwa umaarufu wa Trump kushinda kiti cha Georgia.

Katika Jimbo la Carolina Kusini, mgombea wa chama cha Republican Ralph Norman alimshinda mgombea wa chama cha Democratic Archie Parnell katika ngome ya wahafidhina.

Mgombea wa Republican Karen Handel alishinda kwa asilimia 53 huku mgombea wa chama cha Democrat akijipatia asilimia 47.

Spika wa bunge Paul Ryan alimpongeza Bi Handel kwa ushindi huo mgumu.

Chama cha Democratic kilishindwa kwa kura chache katika maeneo ya Kansas na Montana mwaka huu.

Bwana Ossoff alishindwa kupata asilimia 50 ya kura zilizohitajika ili kuibuka mshindi katika uchaguzi wa jimbo la Atlanta mnamo mwezi Aprili, hali hiyo ilipelekea kuitishwa kwa awamu ya pili ya uchaguzi dhidi ya Handel.

Katika jimbo la Georgia matumizi ya uchaguzi huo yalifikia dola milioni 56 ikiwa ndio uchaguzi uliogharamikiwa katika historia ya Marekani.