UFARANSA-SIASA

Mawaziri wapya wateuliwa Ufaransa baada ya watatu kujiuzulu

Waziri Mkuu Edouard Philippe, Alhamisi, Mei 18, 2017, Matignon.
Waziri Mkuu Edouard Philippe, Alhamisi, Mei 18, 2017, Matignon. RFI/ Pierre René-Worms

Serikali ya pili ya utawala wa Emmanuel Macron imetangazwa mapema siku ya Jumatano jioni, siku moja baada ya mawaziri watatu kutangaza kujiuzulu kwenye nafasi zao serikalini.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya Sylvie Goulard, Waziri wa Jeshi, , François Bayrou, Waziri wa Sheria, na Marielle de Sarnez, waziri wa mambo ya Ulaya, kutangaza kujiuzulu, watu watatu wametangazwa kuchukua nafasi hizo.

Mawaziri wote waliojiuzulu ni kutoaka chama cha MoDem kiliopata viti 24 bungeni. Wakati huo huo Florence Parly ameteuliwa Waziri wa Sheria, Nicole Belloubet, Waziri wa majeshi na Nathalie Loiseau, ameteuliwa Waziri wa Mambo ya Ulaya. Jacques Mézard amechukua nafasi ya Richard Ferrand, aliekua waziri wa Mshikamano. Jacques Mezard, pia ataongoza kundi la wabunge kutoka chama cha rais Emmanue macron cha republique en marche Bunge.

Kama ilivyokuwa ilipotangazwa serikali ya kwanza ya Edouard Philippe, Mei 17, 2017, uteuzi wa timu hii mpya ya mawaziri inasubiriwa kutekeleza majukumu yake. Katika mazungumzo ya siri, timu ya Waziri Mkuu Edouard Philippe na rais Emmanuel Macron iliandaa serikali yenye wajumbe 28.

Baada ya chama cha Republique en marche na washirika wake kufanikiwa katika uchaguzi wa wabunge wa tarehe 11 na 18 Juni, kama ilivyo kawaida, Waziri Mkuu aliwasilisha barua yake ya kujiuzulu.

Mawaziri watatu waliojiuzulu ni kutoka chama cha MoDem, kinachokabiliwa na uchunguzi kuhusu mazingira ya ajira ya wasaidizi wake katika bunge la Ulaya.