MALI-SIASA

Serikali ya Mali yaahirisha kura ya maoni kuhusu marekebisho ya katiba

Rais Ibrahim Boubacar Keita hajaeleza sababu ya kuahirisha kura ya maoni kuhusu marekebisho ya katiba..
Rais Ibrahim Boubacar Keita hajaeleza sababu ya kuahirisha kura ya maoni kuhusu marekebisho ya katiba.. AFP PHOTO / HABIBOU KOUYATE

Serikali ya Mali imetangaza kuahirisha kura ya maoni iliyokuwa imepangwa kufanyika tarehe 9 mwezi ujao, kuibadilisha katiba ya nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Marekebisho hayo yanalenga kumwongezea mamlaka rais lakini pia kuundwa kwa majimbo mapya kw amujibu wa mkataba wa amani uliotiwa saini katinya serikali ya Bamako na waasi Kaskazini mwa nchi hiyo mwaka 2015.

Kura ya maoni ilikua ilipangwa kufanyika tarehe 9 Julai, kuhusu rasimu mpya ya marekebisho ya Katiba. Zoezi hilo limeahirishwa lakini haijulikani litafanyika lini. Uamuzi huo ulitolewa na Baraza la mawaziri chini ya uenyekiti wa rais wa Mali Ibarahi Boubacar Keita.

Hakuna sababu zilizotolewa kuhusu kuahirishwa kwa zoezi hilo, lakini inajulikana kwamba Mahakama ya Katiba inajiandaa kutoa maoni yake kuhusu kufayika kwa kura hii ya maoni.

Alhamisi, hii Juni 22, vijana wa kijiji cha Sikasso, kusini mwa mji wa Bamako, walikua walipanga kufanya maaandamano ya amani dhidi ya kura hiyo ya maoni. Baada ya kutangazwa kuahirishwa kwa kura ya maoni, maandamano hayo yalifutwa kabla ya ya kutangazwa baadae kwamba yatafanyika.

Rais Ibrahim Boubacar Keita hajaeleza sababu ya kuahirisha zoezi hilo lakini wachambhzi wa siasa wanasema huenda ni kwa sababu ya maandamano ya wapinzani wanaopinga mabadiliko hayo ya katiba.