Gurudumu la Uchumi
Ubunifu wa mafazi unavyoweza kuongeza pato la mtu na kukuza uchumi
Imechapishwa:
Cheza - 10:07
Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili, imekutana uso kwa uso na mbunifu maarufu wa nguo nchini Tanzania, Manju David Msita, mbunifu mkongwe anaefanya kazi ya kipekee katika ubunifu wa mavazi, anasema yeye haigi lakini ana buni.Mtayarishaji wa makala haya Emmanuel Makundi amezungumza na Manju kwa kina kuhusiana na sanaa ya ubunifu na namna inavyoweza kutumiwa na wabunifu hasa vijana kujipatia kipato na kukuza uchumi wa nchi kupitia sanaa hii.Waweza kuwasiliana na Manju Msita kwa Instgram/Facebook na barua pepe, manjumsita@yahoo.com/ smartafrika@yahoo.com au kwa namba +255 0655 411 441