Pata taarifa kuu
ANGOLA-UCHAGUZI-SIASA

Rais Mpya wa Angola João Lourenço atawazwa

João Lourenço katika mkutano na waandishi wa habari mjini Luanda tarehe 22 Agosti 2017.
João Lourenço katika mkutano na waandishi wa habari mjini Luanda tarehe 22 Agosti 2017. REUTERS/Stephen Eisenhammer

Rais mpya wa Angola João Lourenço ameapishwa Jumanne hii, Septemba 26 mbele ya maelfu ya watu na marais kadhaa. Lakini mtangulizi wake, Jose Edouardo Dos Santos, anaendelea kiuwa na ushawishi mkubwa katika utawala wake na chama tawala.

Matangazo ya kibiashara

João Lourenço ameapishwa mbele ya maelfu ya watu waliokusanyika katika Uwanja wa Uhuru. Marais wengi walikuwepo katika sherehe hizo: Rais wa Ureno, pamoja na marais kadhaa kutoka Afrika kama rais wa DR Congo Joseph Kabila na Denis Sassou-Nguesso wa Congo Brazzaville, rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma na rais wa Guinea Alpha Condé, ambaye pia ni mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika.

Mtangulizi wa João Lourenço, José Manuel Dos Santos alikuwa mmoja wa viongozi wa mwisho kuwasili kwenye eneo la sherehe, baada ya kuondoka ikulu kama mkuu wa nchi kwa mara ya mwisho. Rais wa zamani alionekana ni mwenye tabasamu,huku akikosoa baadhi ya maafisa wa itifaki yake.

Baada ya kuapishwa rasmi rais mpya Lourenço na Makamu wa wake, mkuu wa zamani wa nchi ya Angola aliomkabidhi kijiti kama ishara ya kumkabidhi uongozi wa nchi. Ishara ya kawaida lakini ya kihistoria, baada ya miaka 38 ya kuiongoza Angola.

"Nitakuwa rais wa wananchi wote wa Angola," alisema João Lourenço. Aliwamewatolea wito wananchi wa Angola kushirikiana, na kuweka kando tofauti tofauti zao za kisiasa, kikanda au kijamii. "Maslahi ya taifa lazima yawe juu zaidi ya maslahi ya makundi yoyote au mtu binafsi," amesisitiza kabla ya kurejelea vipaumbele vyake: mapambano dhidi ya umaskini, kuongeza uchumi na kuimarisha demokrasia. Pia ametoa wito kwa asasi za kiraia kushirikiana zaidi na ameahidi hasa kwamba utawala hautaingilia kazi za vyombo vya habari.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.