UFARANSA-EU-MAENDELEO-UCHUMI

Emmanuel Macron apendekeza mipango yake kwa Ulaya

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, wakati wa hotuba yake kwa Ulaya aliyoitoa katika Chuo Kikuu  cha Sorbonne, Paris tarehe 26 Septemba 2017.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, wakati wa hotuba yake kwa Ulaya aliyoitoa katika Chuo Kikuu cha Sorbonne, Paris tarehe 26 Septemba 2017. REUTERS/Ludovic Marin/Pool

Katika hotuba yake katika Chuo Kikuu cha Sorbonne, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aliwasilisha mapendekezo yake siku ya Jumanne (Septemba 26) kwa minajili ya kufufua mpango wa Ulaya.

Matangazo ya kibiashara

"Ulaya tunayojua ni dhaifu sana, ni haipigi hatua, pia haitoshi, lakini Ulaya peke yake inaweza kutupa uwezo wa kufanya kazi duniani dhidi ya changamoto kubwa zinazotukabili," alisema Emmanuel Macron katika wakati akianza kutoa hotuba yake katika Chuo Kikuu cha Sorbonne.

■ Kwenye nyanja ya ulinzi na usalama

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ametoa wito wa kutaka kubuniwa kikosi cha pamoja cha jeshi kama sehemu ya maono yake ya siku za usoni kwa muungano huo.

Bwana Macron alipendekeza kuwa kikosi hicho kipya kitakuwa ni sehemu ya Nato.

Rais Emmanuel Macron alisema anataka mungano wa Ulaya kuboresha mifumo yake ya ulinzi kwa kubuni jeshi la pamoja.

Hakutoa taarifa zaidi lakini alisema kuwa kikosi hicho kitakuwa sehemu ya Nato na kinatajiwa kuanza huduma ifikapo mwaka 2020.

Nchi kadha za Muungano wa ulaya sawa na kamishina wa tume ya Ulaya Jean-Claude Juncker, awali wamesema kuwa kunastahili kuwepo jeshi la pamoja na Ulaya kukabiliana na Urusi na vitisho vingine.

Kufuatia vimbunga ambavyo hivi karibuni vilisababisha madhara makubwa katika eneo la Caribbean, rais wa Ufaransa pia aliaomba kuundwa kwa kikosi cha pamoja cha ulinzi wa raia dhidi ya majanga ya asili.

■ Kwenye nyanja ya uhamiaji

"Mgogoro wa wahamiaji ni changamoto ya kudumu. Tunakosa uwezo na ubinadamu, "alisema Emmanuel Macron. Ili kurekebisha hali hii, alipendekeza kuundwa kwa ofisi ya hifadhi ya Ulaya ili kuharakisha na kuunganisha taratibu, kuundwa kwa polisi ya mipaka ya Ulaya.

Rais wa Ufaransa pia anataka kuanzishwa kwa "mshikamano" kwa mpango wa mafunzo na ushirikiano wa wakimbizi.

■ Kwenye nyanja ya uchumi

Emmanuel Macron alipendekeza kuwa eneo la nchi zinazotumia euro linapaswa kuwa na bajeti yake na Bunge lake.