URUSI-MAREKANi-TWITTER-UCHAGUZI

Twitter: Urusi ilijaribu kuingilia uchaguzi wa Marekani

Baadhi ya ujumbe wa barua pepe ambao mwana wa kwanza wa Donald Trump alichapisha kwenye Twitter.
Baadhi ya ujumbe wa barua pepe ambao mwana wa kwanza wa Donald Trump alichapisha kwenye Twitter. DonaldJTrumpJR/Handout via REUTERS

Mtandao wa kijamii wa Twitter, umebaini kuwa kulikuwa na matangazo 2,000 yaliyotumiwa na vyombo vya Habari nchini Urusi kujaribu kuingilia Uchaguzi wa Marekani mwaka uliopita.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa kutoka kampuni ya Twitter imeleeza kuwa vyombo vya Habari vilitumia karibu Dola za Marekani 274,000 kuingilia Uchaguzi wa Marekani.

Urusi imekuwa ikishtumiwa kwa kuingilia Uchaguzi wa Marekani, madai ambayo ameyakanusha.

Siku ya Jumatano wiki hii rais wa Marekani Donald Trump alishtumu mtandao wa Facebook kuwa ni mtandao wa kijamii "dhidi ya Trump" na kuhoji jukumu la mtandao huo wakati wa kampeni za urais mwaka 2016.

Katika ujumbe huo, Donald Trump alistumu gazeti la New York Times na Washington Post kuwa dhidi yake na kujiuliza juu ya uwezekano wa "njama" ya vyombo vya habari dhidi yake.

Mwanzilishi huyo wa Facebook Mark Zuckerberg, amebainisha kuwa wakati wote wa uchaguzi mtandao wake ulifanya unachoweza kwa manufaa ya wapiga kura.

Hivi punde Facebook itawasilisha matangazo ya kisiasa 3,000 kwa wachunguzi wa serikali wanaochunguza tuhuma za Urusi kuingilia uchaguzi mkuu wa Marekani.

Mtandao huo unaamini huenda matangazo hayo yalinunuliwa na mashirika ya Urusi wakati na baada ya uchaguzi huo wa urais 2016.

Mitandao ya Facebook, Twitter na Google imeombwa kutoa ushahidi mbele ya kamati ya kijasusi ya baraza la senetila Marekani Novemba 1 kuhusu tuhuma za Urusi kuingilia katika uchaguzi wa Marekani.

Katika siku za nyuma, Donald Trump alikaribisha kazi kubwa inayofanywa na mtandao wa Facebook na hata kusema kuwa mtandao huo wa kijamii ulimsaidia kushinda uchaguzi wa urais.