Mfalme wa Morocco awafuta kazi mawaziri watatu baada ya mgogoro katika jimbo la Rif
Imechapishwa:
Mfalme wa Morocco Mohammed Mohamed wa 6 amewafuta kazi mawaziri wake watatu akiwashtumu kuchelewesha maendeleo ya kiuchumi katika jimbo la Rif, kaskazini mwa nchi hiyo.
Mawaziri hao waliofutwa kazi ni pamoja na Mohamed Hassad, Waziri wa Elimu, ambaye alilikuwa wakati wa kusainiwa kwa mkataba wa mpango huu mwezi Oktoba 2015 Waziri wa Mambo ya Ndani, pamoja na Mawaziri wa Afya Houcine El Ouardi na wa Makazi Nabil Benabdellah.
Jumamosi iliyopita, Mfalme Mohammed VI alikuwa ametishi kuwafukuza kazi mawaziri hawa kosa la "kutekeleza" ndani ya muda uliyotolewa miradi mbalimbali katika mji wa Al-Hoceima.
Jimbo la Rif lilishuhudia maandamano mwaka jana ambayo yalisababishwa na kifo cha muuza samaki katika makabiliano na polisi. Tukio hili liliashiria matumizi ya nguvu kupita kiasi, rushwa na hali ya kutojali.
Mfalme Mohammed wa 6 amekua akiwalaumu maafisa wa serikali kushindwa kutekeleza miradi ya maendeleo katika jimbo la Rif.