MAREKANi-UCHUMI

"Paradaise Papers": Kashfa mpya ya ushuru yafichuliwa

"Paradise Papers" yaweka wazi mifumo ya ukwepaji kodi ambapo makampuni mengi yananufaika.
"Paradise Papers" yaweka wazi mifumo ya ukwepaji kodi ambapo makampuni mengi yananufaika. Getty Images/Linda Raymond

Baada ya faili ya "Panama Papers " kufichuliwa na kuhusisha viongozi mbalimbali duniani, faili inayofuata inayogonga vichwa vya habari nchini Marekani ni ile ya "Paradise Papers", Nyaraka za Paradizo, ambapo Waziri wa Biashara wa Marekani anahusishwa.

Matangazo ya kibiashara

Shirikisho la Kimataifa la Waandishi wa habari wanaohusika na masuala ya uchunguzi na vituo vya habari zaidi ya mia moja duniani walichapisha siku ya Jumapili uchunguzi mpya kuhusu faili hii. Nyaraka hizo ambazo zimekabidhiwa kundi la mashirika ya habari, zinaonesha kuwa Waziri wa Biashara wa Marekani Wilbur Ross aliendelea kuwa na maslahi katika kampuni ya usafirishaji wa mafuta na gesi iliyokuwa ikihudumia kampuni ya kawi ya Urusi, Sibur.

Zaidi ya faili milioni 13 ikiwa ni pamoja na vifungo 19 vya kodi, ambavyo vimefichuliwa tayari viewahusisha viongozi kadhaa duniani ikiwa ni pamoja na mashirika mbalimbali. Miongoni mwa faili zilizofichuliwa na vyombo vya habari, kumeonekana majina ya wanasiasa 120 ikiwa ni pamoja na viongozi mbalimbali duniani. Malkia wa Uingereza, Elizabeth II, auwashirika wa karibu wa Donald Trump ni miongni mwa viongozi waliotajwa.

Waziri wa Biashara wa Marekani, Wilbur Ross, anaendelea kufanya biashara na washirika wa karibu wa Vladimir Putin licha ya vikwazo vya Marekani dhidi ya Urusi. Kupitia mfululizo wa uwekezaji katika makampuni ya Urusi, anamiliki hisa katika kampuni ya Navigator, mshirika wa kampuni ya kawi ya Urusi Sibur, ambayo ni sehemu mali ya mkwe wa Vladimir Putin, Kirill Shamalov.

Seneta wa chama cha Democratic Richard Blumenthal amesema Bw Ross aliambia Bunge la Congress kwamba hakuwa tena na hisa katika kampuni hiyo kwa jina Navigator.

Wizara ya uchumi Marekani imesema Ross hakufanya jambo lolote ambalo ni kinyume cha sheria na kwamba hajawahi kukutana na Warusi hao ambao wamewekewa vikwazo na Marekani.

Jina la Waziri wa Mambo ya Ne wa Marekani, Rex Tillerson, pia limeonekana katika faili hii ya "Paradise Papers", kama mkurugenzi wa kampuni iliyosajiliwa Bermuda kwa kuuuza na kuknunua mafuta Yemen, wakati alikua akifanya kazi kwa kampuni ya ExxonMobil. ambayo aliongoza tangu mwaka 2006 hadi 2016.

Pia kuna majina ya viongozi mbalimbali ambao ni washirika wa karibu wa Rais wa Urusi Vladimiri Putin, ikiwa ni pamoja na mawaziri, washauri, wafadhili wa kampeni yake, ambao wana mali nyingi katika baadhi ya makamuni," amesema Cécile Prieur, mhariri wa gazeti la Le Monde, ambaye alishiriki katika utafiti huu.