MISRI-SISSI-UCHAGUZI-SIASA

Abdel Fattah al Sissi : Sina nia ya kuwania zaidi ya mihula miwili

Abdel Fattah al Sissi anakosolewa kuminya upinzai nchini Misri.
Abdel Fattah al Sissi anakosolewa kuminya upinzai nchini Misri. AFP PHOTO / KHALED DESOUKI

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi, ambaye bado hajatangaza rasmi kama atawania katika uchaguzi wa mwaka ujao, amekiambia kituo cha habari cha Marekani cha CNBC kuwa hana nia yoyote ya kubadili katiba ya nchi kwa lengo la kuwania muhula wa tatu.

Matangazo ya kibiashara

"Siwezi kufikiria kusalia madarakani siku moja zaidi dhidi ya matakwa ya Wamisri," Bw Sissi amesema katika mahojiano na CNBC. Abdel Fattah al Sissi, ameendelea kukosolewa na wapinzani wake pamoja na watetezi wa haki za binadamu kwa kuuminya upinzani.

"Hatutabadili (Katiba). Niko tayari kuhudumu kwa mihula miwili pekee ya miaka minne kwa kila muhula," ameongeza rais wa Misri.

Abdel Fattah al Sisi alichaguliwa kuwa rais wa Misri mwaka 2014 baada ya kumpindua aliyekua rais wa nchi hiyo, Mohamed Morsi, baada ya maandamano makubwa dhidi ya utawala wake.

angu wakati huo ameminya vyama vya upinzani na mashirika ya kiraia yanayomkosoa na inaonekana kuwa hatakabiliana na upinzani mkubwa kama atawania katika uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika mwezi Machi au Aprili 2018.