AFRIKA KUSINI-ZUMA-UFISADI

Jacob Zuma aendelea kukabiliwa na shutma za ufisadi

Taarifa mpya kutoka nchini Afrika kusini zinasema kuwa kitabu kipya chenye utata kuhusu madai kuwa rais Zuma amejilimbikizia fedha nyingi zinasema kuwa huenda kikazusha utata zaidi baada ya wataalamu wa kiusalama kukifuatilia kwa undani.

Jacob Zuma aendelea kusakamwa Afrika Kusini.
Jacob Zuma aendelea kusakamwa Afrika Kusini. REUTERS/James Oatway
Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati Majasusi wa Afrikia Kusini wanataka kufutiliwa mbali kwa kitabu hicho,wakisema kuwa kitabu hicho kimajaa makjosa na kinakiuka sheria ya ujasusi.

Kitabu hicho kinadai kwamba Zuma kwa muda wa miezi minne alipokea mshahara kutoka kwa mfanyibiashara mmoja mbali na mshahara anaolipwa na serikali na kwamba hakuutangaza mshahara huo kwa watoza ushuru wa taifa hilo.

Liesl Louw-Vaudron ambaye ni mtaalamu wa usalama na kisiasa ameiambia RFI kuwa huenda kitabu hicho kikazua utata zaidi.

Baada ya nakala za kitabu hicho kuchapishwa siku ya Jumapili katika gazeti moja, msemaji wa Jacob Zuma alitoa taarifa ,akikana makosa yoyote dhidi ya rais Zuma.

Rais Zum aeameendelea kukabiliwa na shutma mbalimbali kuhusiana na ubadhirifu wa mali ya umma.