MAREKANI-AFYA

Mvutano dhidi ya mageuzi ya kodi Marekani

Maandamano dhidi ya mageuzi ya kodi yaliyopendekezwa na kambi ya Donald Trump yaifanyika Washington tarehe 15 Novemba 2017.
Maandamano dhidi ya mageuzi ya kodi yaliyopendekezwa na kambi ya Donald Trump yaifanyika Washington tarehe 15 Novemba 2017. REUTERS/Aaron

Rais wa Marekani Donald Trump anakutana Alhamisi hii, Novemba 16 na wabunge kutoka chama cha Republican kuwashawishi kupitisha mageuzi ya kodi haraka iwezekanavyo. Mpango huu ambao unatazamia kupunguza kodi kubwa ni kipaumbele kwa utawala wa Donald Trump.

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumanne Maseneta walirekebisha nakala hii ili kuingiza kipengele cha kufutwa kwa sehemu ya Sheria ya Afya iliyowekwa chini ya utawala wa Barack Obama, hali ambayo imezua hasira kwa upande wa chama cha Democrat. Siku ya Jumatano, maandamano ya wapinzani wa mpango huo yalifanyika mbele ya bunge la Congress.

Mamia ya waandamanaji walikusanyika mbele ya bunge la Congress kupinga dhidi ya muswada wa mageuzi ya kodi. Catherine Landfill, mwanasheria, alitumia muda wake wa mapumziko kuja kuandamana na wengine.

"Muswaa huu hutoa zawadi kubwa ya kodi kwa Wamarekani tajiri zaidi, kupitia migongo ya watu masikini zaidi, na hiyo ni hatari sana kwa muswada huu, ambo unaitwa kashfa ya Trump, " amesema Catherine Landfill.

Muswada huu unatazamia kupunguza kodi kwa makampuni kutoka 35% hadi 20%. "Mageuzi haya ya kodi hayaeleweki na yanaongeza upungufu fulani. Hatuwezi kuwaacha wafanye hivyo! ", Nancy Pelosi, kiongozi wa kundi la wabunge kutoka chama cha Democrat, amepinga.

Muswada huu pia unatazamia kufuta ibara muhimu ya Sheria ya Afya iliyowekwa chini ya utawala wa Barack Obama: wajibu wa kuchukua bima ya afya au kulipa faini. "Ni ajabu," alisema Chuck Schumer, Kiongozi wa kundi la Maseneta kutoka chama cha Kidemocrat, huku akibaini kwamba Wamarekani milioni 13 watapoteza bima yao ya afya. Bei ya bima itaongezeka kwa 10%. Hakuna Mmarekani hata mmoja ambaye anataka hivyo. Kwa hiyo tunapaswa kupambana dhidi ya sheria hii kama tulivyopambana dhidi ya mageuzi yao ya afya. "

Lakini Wabunge kutoka chama cha Republican ambao ni wengi katika bunge la Congress wameamua kupitisha muswada huo haraka iwezekanavyo. Wana mahitaji muhimu ya kuchapisha angalau moja ya mafanikio makubwa ya kisheria.