UJERUMANI-SIASA

Mazungumzo ya kuunda serikali ya mseto yavunjika Ujerumani

Angela Merkel Novemba 19, 2017 katika makao makuu ya chama cha CDU wakati wa mazungumzo ili kuunda serikali ya mseto.
Angela Merkel Novemba 19, 2017 katika makao makuu ya chama cha CDU wakati wa mazungumzo ili kuunda serikali ya mseto. REUTERS/Axel Schmidt

Nchini Ujerumani, mazungumzo yaliyoongozwa na Angela Merkel kuunda serikali ya mseto kati ya chama cha Conservative na chama chenye mrengo wa kati cha Centrist Free Democrats na vyama vingine katika mazungumzo yameumbulia patupu.

Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo hayo yamevunjika baada ya chama chenye cha FDP kujitoa kwenye mazungumzo hayo kikilalamikia tofauti zisizoweza kusuluhishwa na chama cha Merkel cha Christian Democrats.

"Ni bora kutokua katika utawala kuliko kutawala vibaya, " kiongozi wa chama cha FDP Christian Lindner amesema, huku akibaini kwamba amependelea kutangaza kujitoa kwenye mazungumzo na chama cha Conservative na vyama vingine katika mazungumzo, akisema kuwa hakuna uaminifu wa kutosha kati ya vyama ili kuunda serikali ya mseto.

Bibi Merkel ameonya kuwepo kwa magumu katika wiki zijazo.

Baada ya wiki ya kadhaa za mazungumzo, nyaraka za kazi zilizotolewa leo zina utata mkubwa, maswali ya wazi na migogoro kuhusu malengo yanayotakiwa kufikiwa. Lakini hakuna maendeleo yoyote ambayo yamepatikana kwa leo. Kinyume chake, baadhi ya maelewano ambayo yalipatikana yamewekwa hatarini, amesema Bw Lindner.