ZIMBABWE-UCHAGUZI-SIASA

Zanu-PF kumfungulia mashitaka Mugabe

Rais Robert Mugabe akikutana na mkuu wa majeshi Jenerali Constantino Chiwenga na maafisa wengine waandamizi katika jeshi la Zimbabwe, ikulu Harare.
Rais Robert Mugabe akikutana na mkuu wa majeshi Jenerali Constantino Chiwenga na maafisa wengine waandamizi katika jeshi la Zimbabwe, ikulu Harare. ©ZIMPAPERS/Joseph Nyadzayo/Reuters

Kiongozi wa chama tawala Cha ZANU PF anabaini kwamba utaratibu wa kumshtaki Rais Robert Mugabe utaendelea siku ya Jumane kama ilivyopangwa, kwa mujibu wa mtandao wa Twitter unaofuatilia taarifa za vyombo vya habari nchini Zimbabwe.

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumapili chama cha Zanu-PF kilitoa muda wa makataa wa kujiuzulu kw rais Mugabe ambao ni Jumatatu kabla ya saa sita mchana

Wananchi wa Zimbabwe walikuwa wanatarajia kwamba rais Robert Mugabe atatangaza kujiuzulu alipohutubia taifa siku ya Jumapili usiku Wengi wanasema hotuba ya Bw. Mugabe imewaacha vinywa wazi.

Katika hotuba yake ya kwanza kwa taifa tangu jeshi lichukue madarakwa Jumatano, Mugabe hakujiuzulu na alisema kuwa ameazimia kuongoza mkutano mkuu wa chama cha Zanu-PF mwezi ujao.

Awali vyanzo vilivyo karibu na Robert Mugabe vilikua vilibaini kwamba alikubali kuondoka mamlaka.

Jeshi linatarajia kufanya mkutano na waandishi wa habari Jumatatu hii asubuhi pamoja na Muungano wa Wapiganaji waliopigania Uhuru wa Zimbabwe.

Awali muungano huu wa maveterani wa vita vya uhuru wa Zimbabwe ulimtaka rais Mugabe kujiuzulu.

Mkutano wa dharura wa Zanu-PF ulimfukuza Bw Bugabe kwenye uongozi wa chama hicho, na kumteuwa aliye kuwa makamo wake Emmerson Mnangagwa kuwa kiongozi wa chama hicho na kupeperusha bendera ya chama cha Zanu-PF katika uchaguzi wa mwaka 2018.