ZIMBABWE-SIASA-USALAMA

Emmerson Mnangagwa amuomba rais Mugabe kujiuzulu

Emmerson Mnangagwa, aliekuwa makamu wa rais wa Zimbabwe, kabla hajatimuliwa kwenye wadhifa huo wiki mbili zilizopita..
Emmerson Mnangagwa, aliekuwa makamu wa rais wa Zimbabwe, kabla hajatimuliwa kwenye wadhifa huo wiki mbili zilizopita.. REUTERS/Philimon Bulawayo

Katika taarifa iliyopelekwa kwa waandishi wa habari, aliekuwa makamu wa rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa, ambaye alitimuliwa mamlakani wiki mbili zilizopita, amesema kuwa "hayuko tayari kurejea nchini wakati ambapo atakua bado hajahakikishiwa usalama wake".

Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo Chama ch Zanu-PF kinatarajia hivi leo kuanzisha mchakato wa kumngoa Robert Mugabe mamlakani.

Afisa wa Zanu-PF amesema kuwa hoja ya kumnyang'anya urais itawasilishwa bungeni leo Jumanne na mchakato wa kumng'oa madarakani unaweza kuchukua siku mbili tu.

Mashtaka yaliyomo kwenye hoja hiyo ni pamoja na kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 93 "kumpa madaraka makubwa ya kikatiba mkewe Grace, na kushindwa kuheshimu katiba''.

Emmerson Mnangagwa, mwenye umri wa miaka 75, aliachishwa kazi tarehe 6 Novemba na kulazimika kukimbilia uhamishoni baada mvutano na mkewe rais Mugabe, Grace Mugabe, mwenye umri wa miaka 52, ambaye alifanikiwa kumuondoa hasimu wake katika kinyang'anyiro cha kumrithi mumewe.

Tangu wakati huo, jeshi limekua na mazungumzo na rais Mugabe anaekataa kujiuzulu licha ya shinikizo kutoka pande mbalimbali nchini Zimbabwe.

Katika hotuba yake kwenye televisheni, Jenerali Chiwenga alisema ameridhishwa na "maendeleo mapya" tangu mapinduzi ya kijeshi wiki iliyopita, hususan "mawasiliano kati ya rais Mugabe na aliyekua makamu wake Emmerson Mnangagwa, ambaye anatarajiwa hivi karibuni nchini Zimbabwe".