SUDAN-URUSI-USHIRIKIANO

Omar al-Bashir kuzuru Urusi licha ya waranti wa kukamatwa

Rais wa Sudan Omar al-Bashir katika mahojiano kituo cha televisheni cha Urusi, Russia Today, Khartoum Desemba 2014.
Rais wa Sudan Omar al-Bashir katika mahojiano kituo cha televisheni cha Urusi, Russia Today, Khartoum Desemba 2014. REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah

Rais wa Sudan Omar al-Bashir ambaye anatafutwa na mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, anatarajiwa Alhamisi, Novemba 23 nchini Urusi. Rais wa Sudan atafanya ziara yake ya kwanza rasmi nje ya nchi tangu nchi yake kufutiwa vikwazo na Marekani. Atapokelwa katika ilkulu ya Kremlin na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa hii ilitolewa na mamlaka ya Sudan na kuthibitishwa mapema wiki hii na ikulu ya Kremlin. Omar al-Bashir anatarajiwa Alhamisi hii mjini Moscow na anapaswa kukutana kwa mazungumzo na rais wa Urusi.

Mikataba ya ushirikiano inaweza kusainiwa pamoja na mikataba katika sekta ya madini, kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje ya Sudan.

Ziara hii ambayo ilipangwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu, itakua ni ziara kwanza ya Omar al-Bashir nchini Urusi.

Licha ya waranti mbili za kukamatwa zilizotolewa na Mahakam ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) dhidi yake, hakuna uwezekano wowote wa rais Bashiri kukamatwa na polisi wa Urusi. Russia haijawahi kusaini Sheria ya Roma inayounda Mahakam ya Kimataifa ya Uhalifu.

Aidha, Moscow ilifuta saini yake kwenye Sheria ya Roma mnamo mwezi Novemba 2016 kufuatia ufunguzi wa uchunguzi wa vita vya mwaka 2008 kati ya Urusi na Georgia. Hatimaye, Vladimir Putin anatarajia kuendeleza uhusiano wa biashara na kisiasa kati ya nchi yake na Sudan.