DRC-UDPS-SIASA

Chama cha UDPS chaendelea kukumbwa na malumbano ya ndani DRC

Wanasiasa wa chama kikuu cha upinzani nchini DRC wanaomuunga mkono Felix Tshisekedi, wanasema hawatambui mkutano mkuu uliofanywa na wanachama wa zamani wa chama hicho mwishoni mwa wiki iliyopita na kumchagua Waziri Mkuu Bruno Tshibala kuwa kiongozi mpya wa chama hicho.

Mbele ya makao makuu ya ya chama cha upinznai cha UDPS, DRC.
Mbele ya makao makuu ya ya chama cha upinznai cha UDPS, DRC. RFI/Habibou Bangré
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo umekigawa chama hicho ambacho kilikuwa kinaongozwa kwa muda mrefu na Etienne Tshisekedi aliyefariki dunia mapema mwaka huu.

Tshibala amesema atafanya kila kilicho ndani ya uwezo wake kurejea katika Ofisi ya chama hicho.

Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Reuben Mikindo, amesema hawamtambui Tshibala kama mwanachama wa chama chao baada ya kumfukuza.

Mapema wiki jana Bruno Tshibala anayesisitiza kuwa yeye ndiye Katibu Mkuu wa chama hicho alisema hivi karibuni, ataitisha mkutano mkuu wa chama hicho ili kumpata kiongozi mpya.

Mvutano umeshika kasi katika chama hicho cha upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuwania mrithi wa mwenyekiti wa chama hicho Etienne Tshisekedi aliefariki miezi kadhaa iliyopita.

Kwa muda wa siku tatu Waziri mkuu wa DR Congo Bruno Tshibala pamoja na wafuasi wa chama hicho walioungana naye wanakutana katika kongamano maalum kwa ajili ya kujiandalia uchaguzi.

Bruno Tshibala alisema chama cha UDPS sio taasisi ya jadi ambayo mtoto anamrithi baba yake.