AFRIKA KUSINI-ZUMA-UFISADI

Zuma atakiwa kuwasilisha utetezi wake kuhusu ufisadi hadi Januari 31

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akabiliwa na kashfa za rushwa nchini mwake.
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akabiliwa na kashfa za rushwa nchini mwake. PHILL MAGAKOE / AFP

Viongozi wa Mashtaka nchini Afrika Kusini wamesema wametoa muda zaidi kwa rais Jacob Zuma, kuwasilisha utetezi wake kuhusu kufunguliwa kwake la mashitaka ya ufisadi.

Matangazo ya kibiashara

Zuma amepewa hadi tarehe 31 mwezi Januari mwaka 2018, kuwaridhisha viongozi wa mashtaka wasimfungulie mashtaka hayo.

Rais Zuma, anadaiwa kuhusika katika visa 783 za ufisadi zenye thamani ya Dola za Marekani Bilioni 2.20 katika mkataba wa kununua silaha alipokuwa Waziri miaka 1990.

Viongozi wa mashtaka walilazimika, kusitisha mpango wa kumfungulia Zuma kesi alipokuwa anajiandaa kuwania uraia mwaka 2009.

Hata hivyo, rais Zuma ameendelea kukanusha madai ya ufisadi dhidi yake.

Rais Zuma, anaandamwa wakati huu anapokaribia kuondoka madarakani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2019.

Wiki hii, rais Zuma atamaliza muda wake katika mwenyekiti wa chama tawala ANC, nafasi ambayo huenda ikachukuliwa na naibu wake Cyril Ramaphosa ambaye pia amekuwa akimshutumu Zuma kwa kuhusika na ufisadi.